Tuesday, September 29, 2015
MAKANISA MENGINE MATATU YAVUNJWA NA KUCHOMWA MOTO.
Do you like this story?
Mfululizo wa uhalifu dhidi ya makanisa mbalimbali bado
unaendelea katika Mkoa wa Kagera ambapo makanisa matatu yamevunjwa na samani
zake kuchomwa moto ndani ya siku moja likiwa ni tukio la pili kutokea katika
kipindi cha wiki mbili sasa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi Augustino Ollomi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na
kwamba jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi kuhakikisha linawatia
mbaroni wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.
Makanisa yaliyoguswa na uhalifu huo ni pamoja na Kanisa la
Kilutheri la Katoro na lile la kijiji cha Musira ,pamoja na kigango cha
Katoliki cha kijiji cha Kituntu katika tarafa ya Katoro.
Uhalifu huo umefanyika kwa staili ya kuvunja milango na
kuchoma samani za ndani ,tofauti na uhalifu wa wiki iliyopita ambapo
makanisa matatu ya kipentekoste yalichomwa moto na kuteketea samani pamoja na
majengo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera SACP Augustino Ollomi
licha ya kuthibitisha kutokea kwa uhalifu huo,anaelezea mikakati inayowekwa na
jeshi hilo kuhakikisha uhalifu huo hautokei tena katika nyumba za ibada.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo John Mongella,ametoa tamko mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa juu ya matukio
hayo.
Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki mbili uhalifu
kutokea katika makanisa ,ambapo September 22 makanisa matatu ya kipentekoste
katika manispaa ya Bukoba yaliteketezwa kwa moto huku watuhumiwa saba
wakishikiliwa kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKANISA MENGINE MATATU YAVUNJWA NA KUCHOMWA MOTO.”
Post a Comment