Wednesday, September 23, 2015

VITUO VYA RADIO NA TV ZOTE NCHINI VYAONYWA NA TCRA




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vituo vya redio na televisheni nchini Tanzania kuepuka kurusha habari za uchochezi hasa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba ameeleza kuwa  vyombo vya habari vinatakiwa kuepuka kurusha na kuandika habari zitakazochochea vurugu na uvunjifu wa amani kwan jamii ina imani kubwa na vyombo vya habari na waandishi wa habari, hivyo hawana budi kutumia weledi katika utoaji wa taarifa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.


Radio 106 na televisheni 28, zimesajiliwa nchini Tanzaia na kwamba katika kuelekea uchaguzi mkuu, tayari vituo vitano vya televisheni vimekuwa na makosa yaliyosababisha kupewa adhabu na onyo.

0 Responses to “ VITUO VYA RADIO NA TV ZOTE NCHINI VYAONYWA NA TCRA”

Post a Comment

More to Read