Tuesday, September 22, 2015
WANAFUNZI SEKONDARI MAGOTO NA MANGA WALALA SAKAFUNI.
Do you like this story?
Wanafunzi wa kidato cha tano na sita
katika shule za Sekondari Magoto na Manga zilizopo katika Wilaya Tarime mkoani
Mara, wamelalamikia kitendo cha kulala sakafuni kwa zaidi ya mwaka moja
sasa huku pia wakikosa chakula na maji.
kali ichukue hatua za haraka za kutatua
tatizo hilo ili wapate huduma bora kwa lengo la kuinua kiwango chao cha elimu.
Wakizungumza mwishoni kwa wiki kwa
nyakati tofauti, baadhi ya wanafunzi ambao waliomba kutotajwa majina yao,
walidai kwamba wamekuwa wakilala sakafuni kwa muda mrefu huku shule hizo
zikishindwa kuwapa chakula na maji kwa ufasaha.
“Tuna shida kubwa katika shule zetu,
tulala chini kutokana na kutokuwapo kwa vitanda kwenye mabweni, pia chakula na
maji ni vya shida,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Aidha, walisema baada ya kuwapo kwa
hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wenzao walijitolea kuuliza uongozi wa elimu wa
wilaya, lakini walijibiwa vitanda vinatengenezwa.
Hata hivyo, walisema mpaka sasa zaidi
ya mwaka mmoja unamalizika hakuna vitanda.
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma
katika shule hizo walidai kushangazwa na hali hiyo licha ya kutoa michango
inayotakiwa na uongozi wa shule hizo.
“Mara kwa mara watoto wetu wanatupigia
simu kutuambia hali ilivyo, pia wanalalamikia kutopata chakula na maji, jambo
linalowafanya wasome kwa shida,” alisema mmoja wa wazazi hao, John Joseph, kwa
niaba ya wenzake.
Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya
Tarime, hakupatikana kuzungumzia malalamiko hayo ya wanafunzi na wazazi.
Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari
Magoto, Anthony Charles, alithibitisha kuwapo kwa tatizo la vitanda na chakula
shuleni hapo.
Charles alisema walitoa zabuni ya
utengenezaji wa vitanda hivyo lakini mpaka sasa havijakamilika.
CHANZO:
NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “WANAFUNZI SEKONDARI MAGOTO NA MANGA WALALA SAKAFUNI.”
Post a Comment