Friday, September 25, 2015

WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA





Taarifa zilizotufikia muda huu kwenye chumba chetu cha habari ni kwamba Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu

Taarifa hizo zimesema Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu

Marehemu Kombani alikuwa akiugua maleria kali
Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu uliowapata

Taarifa zaidi za msiba huo zitakujia hapa hapa

0 Responses to “ WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA”

Post a Comment

More to Read