Thursday, October 22, 2015

.BAADHI YA WANANCHI WAHOFIA UCHAGUZI NA KUHAMA MAKAZI YAO KWA MADAI KUWA MITA 200 MTWARA




Wananchi wa mkoa wa Mtwara wameingia hofu na baadhi yao wameanza kuyakimbia makazi yao wengi wakiwa wanawake na watoto kwa madai nyumba zao zipo ndani ya mita miambili hivyo wanalazimika kuondoka kutii kauli ya serikali.
Wakizungumza na waandishi baadhi ya wananchi wamesema mbali na kutii kauli hiyo wingi wa askari polisi ambao wamesambaa maeneo mbalimbali ya mji wamekuwa wakitia hofu wananchi.

Akizungumzia hofu hiyo mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amesema jeshi la polisi limelazimika kuweka ulinzi huo baada ya kuwapo kwa taarifa za kuandaliwa makundi mbalimbali kuzuia watu kupiga.

Watu laki saba ishirini na nane elfu na mia tisa 81 kutoka majimbo kumi ya mkoa wa Mtwara wanatarajiwa kupiga kura siku ya jumapili kuchagua rais, wabunge na madiwani.

0 Responses to “.BAADHI YA WANANCHI WAHOFIA UCHAGUZI NA KUHAMA MAKAZI YAO KWA MADAI KUWA MITA 200 MTWARA”

Post a Comment

More to Read