Thursday, October 22, 2015

HABARI MOTOMOTO HABARI PICHA SIMBA SAKATA LA NGONGOTI MSENEGALI WA SIMBA 'KUVULIWA HIRIZI' JANA SOKOINE SAKATA LA NGONGOTI MSENEGALI WA SIMBA 'KUVULIWA HIRIZI' JANA SOKOINE






Wachezaji wa Prisons wakimzonga mshambuliaji Msenegali wa Simba SC, Pape Abdoulaye N'daw kumshinikiza avue hirizi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Prisons ilishinda 1-0(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Mwishowe refa alimuamuru N'daw arudi kwenye chumba cha kuvalia akakaguliwe(Picha na David Nyembe wa Fahari News)




N'daw 'akimtisha' mchezaji wa Prisons aliyemshupalia amevaa hirizi(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


N'daw akiingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo ili kukaguliwa wakati ambao mchezo ulisimama kwa dakika nne kipindi cha kwanza






Mchezaji wa Prisons aliyedai N'daw ana hirizi akionywa kwa kadi ya njano kabla ya mchezo kuendelea(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

0 Responses to “ HABARI MOTOMOTO HABARI PICHA SIMBA SAKATA LA NGONGOTI MSENEGALI WA SIMBA 'KUVULIWA HIRIZI' JANA SOKOINE SAKATA LA NGONGOTI MSENEGALI WA SIMBA 'KUVULIWA HIRIZI' JANA SOKOINE”

Post a Comment

More to Read