Monday, October 12, 2015

.NEC YAOMBWA KUWEKA WAZI HATUA ZOTE ZA UPIGAJI KURA HADI MATOKEO


Mkuu wa Mkoa wa Kagera,John Mongella



Katika kuondokana na malalamiko ambayo hujitokeza baada ya  uchaguzi ambayo hupelekea baadhi ya wagombea na  viongozi wa vyama vya siasa kutokubaliana na matokeo hali ambayo wakati mwingine husababisha vitendo vya uvunjifu wa amani, tume ya taifa ya uchaguzi imeombwa kuweka wazi hatua zote zitakazoongoza  mchakato  wa zoezi wa upigaji kura hadi hatua ya kutangaza matokeo.

Ombi hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa kagera,John Mongella kwenye hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maofisa wasimamizi wa uchaguzi wa mikoa ya Geita na Kagera iliyoandaliwa na tume ya taifa uchaguzi na kufanyika kwenye hoteli ya Kolping iliyoko katika manispaa ya Bukoba.

Kwa upande wake,Raphael Nswanzigwanko ambaye ni mratibu wa uchaguzi wa mikoa wa kanda ya ziwa  ameeleza kuwa tume ya taifa ya imejipaga vizuri na itahakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na wa haki, pia amewatahadhalisha wananchi kuwa makini na watakaotoka matokeo  kwa kutuma njia zao amesema tume hiyo ndiyo yenye mamlaka ya  kutangaza matokeo.

Naye, msimamizi wa wa uchaguzi wa mkoa wa Kagera,Fabian Kapucholojiga anaeleza maandalizi ya uchaguzi ambayo yameishafanyika hadi sasa katika mkoa huo, huku Aron Kagulumjuli mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya bukoba, akieleza changamoto ambazo wasimamizi wa uchaguzi hukumbana nazo mara kwa mara ambazo zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

0 Responses to “.NEC YAOMBWA KUWEKA WAZI HATUA ZOTE ZA UPIGAJI KURA HADI MATOKEO”

Post a Comment

More to Read