Wednesday, October 14, 2015

UMOJA WA MATAIFA WAANZISHA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA.




Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh Benard Membe amesema changamoto kubwa inayoikabili umoja wa mataifa ni namna ya kusaidia athari zinazotokana na wakimbizi katika nchi husika pamoja na kufidia watu wanaoathiriwa na wakimbizi.

Mh Membe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya miaka sabini ya umoja wa mataifa ambapo amesema kwa sasa duniani kuna wakimbizi milioni 38 na Tanzania imepokea wakimbizi 169,484 hivi karibuni na kwamba wanapoingia athari ziko nyingi ikiwemo mashule kufungwa ili waweze kuhifadhiwa.

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa akizungumza katika maadhimisho hayo amesema uongozi na utawala bora umechangia kwa kiasi kikubwa Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani na kuongeza kuwa kwa sasa nchi za Afrika zinafanya jitihada kuhakikisha zinadumisha amani ili kuepuka kuzalisha wakimbizi.

Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria maadhimisho hayo wametoa wito kwa tume ya taifa ya uchaguzi kusimamia haki na uadilifu ili Tanzania ibaki kisiwa cha manai hata baada ya uchaguzi na kuwataka watanzania hasa vijana kufuata sheria kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na zoezi la uchaguzi mkuu.

0 Responses to “UMOJA WA MATAIFA WAANZISHA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA.”

Post a Comment

More to Read