Wednesday, October 14, 2015

.RAIS KIKWETE AITAKA TANESCO KUWASHA MITAMBO YOTE ILI KUPATA UMEME WAKUTOSHA.







Serikali kupitia TANESCO imekamilisha miradi mitano na inatekeleza miradi mingine saba ya kufua umeme kwa kutumia nishati ya gesi asilia mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.Kiasi cha umeme unaofuliwa kwa kutumia gesi asilia unafikia megawati 546 na miradi iliyopo kwenye utekelezaji itakapokamilika inatarajiwa kuongeza ufuaji wa umeme kutokana na gesi asilia kufikia megawati 2,475.Miradi  hii ipo kwenye hatua mbalimbali.

Leo Octoba 13 Tanesco ilizindua rasmi mradi huo wa Umeme unaozaliwa kutokana na gesi asilia ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete.

Kukamilika kwa miradi hiyo kutakidhi mahitaji ya umeme nchini na kuondoa utegemezi wa mitambo ya kufua umeme kwa njia ya maji ambayo kiwango cha ufuaji wa umeme kimeshuka kutokana na kushuka kwa kina cha maji kwenye mabwawa, hali ambayo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuendelea kwa shughuli za kibinadamu kwenye mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa hayo.

0 Responses to “.RAIS KIKWETE AITAKA TANESCO KUWASHA MITAMBO YOTE ILI KUPATA UMEME WAKUTOSHA.”

Post a Comment

More to Read