Sunday, February 7, 2016
ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016"
Do you like this story?
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu. |
Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto |
Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza. |
Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo |
Miss
Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano
hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili
kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya
kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na
mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi
katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es
Salaam.
Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha
kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa
Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa
wa MISS ALBINISM 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016"”
Post a Comment