Friday, April 15, 2016
ANNE KILANGO MALECELA AFUNGUKA BAADA YA RAIS KUMSIMAMISHA KAZI YA UKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Do you like this story?
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, ameibukia kanisani na kutoa
ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi
wake.
Kilango,
Jumatatu wiki hii uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka huu, kudai
kuwa mkoa wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata mmoja.
Hata
hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali kuna
watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya za Ushetu na
Shinyanga.
Rais
Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa wafanya
uchunguzi kuhusu uwapo wa watumishi hewa katika mikoa yao na kutoa taarifa.
Kutokana
na kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli
alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa siku 27.
Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo.
Mbali na
Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa hizo za kutokuwapo watumishi hewa
katika mkoa.
Alivyosema
Kanisani
Akiwasalimia
waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga, baada ya kupewa
fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu kwa kila jambo kwa yote
yaliyomtokea.
“Ndugu
waumini wenzangu, hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu
unapojifungua mtoto akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni mapenzi ya
Mungu.
"Ukiona
mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa kumshukuru
Mungu kwa kila jambo,” alisema
kwa maneno mafupi na kisha kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini
wenzake, wakiwamo viongozi wa kanisa.
Alivyoanza
Kazi
Mbele ya
kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya kuanza kazi,
Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi ambazo
atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es Salaam kumwona
mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na pindi hali yake
ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.
Hayo
aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi
25, alisali kanisani hapo.
Sambamba
na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza rushwa
na ufisadi na kurejesha hadhi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.
Kilango
ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake kwa
mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo,
Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko Ikulu ndogo, eneo la
Lubaga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ANNE KILANGO MALECELA AFUNGUKA BAADA YA RAIS KUMSIMAMISHA KAZI YA UKUU WA MKOA WA SHINYANGA ”
Post a Comment