Friday, April 15, 2016
RAIS WA JAMHURI YA SUDANI KUSNI, MHE. SALVA KIRII KUWASILI LEO TANZANIA
Do you like this story?
Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa
Jamhuri ya Sudan Kusini atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania
leo tarehe 15 Aprili 2016.
Rais Kiir anakuja nchini kusaini Mkataba
wa kuwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) ambapo tangazo la kukubaliwa kuwa Mwanachama wa EAC
lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa
Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha mwezi Machi 2016.
Rais Kiir atawasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:00 asubuhi na baadaye ataelekea
Ikulu na kupokelewa na Mwenyeji wake, Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Baada ya hapo, Viongozi hao watashiriki hafla ya uwekaji saini ya Mkataba huo
iliyopangwa kuanza saa 5:00 asubuhi na kisha watapata fursa ya kutoa hotuba na
kusaini Communique.
Rais wa Sudan Kusini atashiriki hafla ya
chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake kabla ya
kuondoka nchini baada ya hafla hiyo.
Sudan Kusini ni nchi ya sita kujiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo inaongeza fursa nyingi za kiuchumi ambazo
zinaweza kuzifaidisha Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania, endapo mipango madhubuti
itawekwa kuzichangamkia. Fursa hizo ni pamoja na za kibiashara kwa kuwa bidhaa
nyingi zinazotumika Sudan Kusini zinaagizwa kutoka Nje ya nchi.
Hivyo, jamii ya wafanyabiashara wa
Tanzania wanahimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini humo na ndani ya
Jumuiya kwa ujumla.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS WA JAMHURI YA SUDANI KUSNI, MHE. SALVA KIRII KUWASILI LEO TANZANIA”
Post a Comment