Saturday, April 23, 2016
OFISI YA WAZIRI MKUU KUTUMIA BAJAJI NA BODABODA.
Do you like this story?
Ofisi ya
Waziri Mkuu itatumia usafiri wa bajaji na bodaboda kuendesha shughuli zake
kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ikiwa ni mkakati wa kubana matumizi wa
Serikali ya Awamu ya Tano.
Mpango huo
umo kwenye hotuba ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyosomwa jana
bungeni na Kassim Majaliwa, na baadaye kusifiwa na mwenyekiti wa Kamati ya
Katiba na Sheria ya Bunge, Mohamed Mchengerwa wakati akisoma maoni ya kamati
kuhusu bajeti hiyo.
Wizara
iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu.
Akiwasilisha
maoni ya kamati hiyo, Mchengerwa alisema uamuzi wa aina hiyo unaendana na dhana
ya kubana matumizi ya fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Hata
hivyo, hotuba iliyosomwa na Waziri Majaliwa haijaeleza pikipiki hizo za
magurumu mawili na matatu zitatumiwa na watumishi wa kada gani.
Serikali
ya Awamu ya Tano imekuwa kwenye mkakati mkali wa kubana matumizi yasiyo ya
lazima na tayari Rais John Magufuli ametangaza kuwa kuanzia mwaka mpya wa fedha
hakuna mtumishi wa umma atakayelipwa zaidi ya Sh15 milioni, huku akifuta
sherehe za maadhimisho ya siku za kitaifa, zikiwamo za Muungano na Uhuru.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
Katika
maoni yake, kamati hiyo imeitaka Serikali kutoa tamko kuhusu maandalizi na
utekelezaji wa mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Pia kamati
hiyo ilitaka Nec kuweka utaratibu mpya wa ratiba ya upigaji kura ili chaguzi
zote za rais, wabunge, madiwani na viongozi wa Serikali za mitaa zifanyike kwa
wakati mmoja.
“Hii
itasaidia kupunguza gharama zinazotumika kwa nyakati mbili tofauti pamoja na
kusaidia kupunguza mtikisiko wa amani nchini,”alisema.
Uchaguzi
wa viongozi wa Serikali za mitaa hutangulia takriban mwaka mmoja kabla ya
Uchaguzi Mkuu ambao huhusisha uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “OFISI YA WAZIRI MKUU KUTUMIA BAJAJI NA BODABODA.”
Post a Comment