Saturday, April 23, 2016
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Khamed Msangi.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
SILAHA MOJA AINA YA SMG NAMBA UA 2911997 PAMOJA NA RISASI 27 KWENYE MAGAZINE |
Pikipiki iliyotumika kufanyia Uhalifu.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
LAKAMATA SILAHA AINA YA SMG NA RISASI ZAKE 27 BAADA YA WATU WANAOSADIKIWA KUWA
MAJAMBAZI KUJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MNAMO TAREHE 18.04.2016
MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MALAMBO, KATA YA RUIWA, TARAFA
YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI
AMBAO IDADI YAO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA WALIFIKA NYUMBANI KWA GERVAS
LAZARO [56] MFANYABIASHARA NA MKE WAKE AITWAE WITNESS MWAKALENGA [50] WOTE
WAKAZI WA MALAMBO KWA LENGO LA KUFANYA UHALIFU WA KUJARIBU KUNYANG’ANYA KWA
KUTUMIA SILAHA.
HATA HIVYO KUTOKANA NA KUWEPO
KWA TAARIFA ZA SIRI KUHUSIANA NA NJAMA NA MPANGO HUO, ASKARI POLISI WALIKUWA
TAYARI ENEO HILO LA TUKIO ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO.
KATIKA KUKABILIANA NA
MAJAMBAZI HAO, BAADHI YA ASKARI WALIIMARISHA ULINZI ENEO HILO NA KUFANIKIWA
KUPATA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.913 CGF AINA YA T-BETTER RANGI
NYEKUNDU AMBAYO ILIKUWA IKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO. BAADA YA UCHUNGUZI PIKIPIKI
HIYO ILIBAINIKA KUWA NA INJINI NAMBA ZJ16ZFNJC2512944 NA CHASSES
LZEPCKLASCL812905 AMBAYO ILITELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO BAADA YA KUONA POLISI WAMEDHIBITI
ENEO HILO.
HATA HIVYO POLISI KWA
KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA ENEO HILO WALIENDELEA KUWAFUATILIA MAJAMBAZI HAO NA
KUFANIKIWA KUPATA SILAHA MOJA AINA YA SMG NAMBA UA 2911997 PAMOJA NA RISASI 27
KWENYE MAGAZINE. AIDHA KATIKA ENEO HILO LA TUKIO AMBALO ILIKUTWA SILAHA HIYO
PIA ILIKUTWA KOFIA MOJA YA KUFICHA SURA [MZURA] ILIYOTELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO
KABLA YA KUKIMBILIA PORINI.
KWA SASA MSAKO /DORIA
INAENDELEA MAENEO YA PORI LA NARCO LILILOPO KATI YA WILAYA YA MBARALI NA
CHUNYA, AMBAPO KIKOSI KAZI CHA ASKARI WA WILAYA HIZO WAMEUNGANA ILI KUWASAKA
MAJAMBAZI HAO KWA AJILI YA KUWAKAMATA. AIDHA TARATIBU ZIMEFANYWA ZA
KUSHIRIKISHA VIONGOZI WA VIJIJI VILIVYOPO MAENEO JIRANI NA MSITU HUO ILI
KUSAIDIANA KUWAPATA MAJAMBAZI HAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI
T.341 BYR IKIWA NA TELA YENYE T.557 BEP AINA YA BEIBEN- TANKER IKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE OSWINI NUNGU [43] MKAZI WA JIJINI DSM IKIWA IMEBEBA SHEHENA YA
MAFUTA AINA YA DIESEL IKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI ZAMBIA ILITEKETEA KWA
KUUNGUA MOTO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO
TAREHE 21.04.2016 MAJIRA YA SAA 15:15 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MALENGA,
KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA CHANZO CHA AJALI HIYO
NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREAK WA GARI HILO NA KUPELEKEA GARI KUUNGUA MOTO.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. THAMANI YA UHARIBIFU BADO
KUFAHAMIKA. UPELELEZI UNAENDELEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI”
Post a Comment