Monday, February 22, 2016

AZAM NA PRISONS ZAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA MCHEZO WA LIGI KUU JUMATANO MBEYA







Tanzania Prisons wakiwa  Mazoezini( Picha na David Nyembe wa Fahari New)






Azam Fc wakiwa katika Mazoezi ( Picha na David Nyembe wa Fahari New)


Joto la mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya na timu ya soka ya Azam FC wenyeji wa Chamanzi jijini Dar es Salaam itakayopigwa katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya siku ya jumatano linazidi panda.

 Timu ya Azam FC imesalia jijini Mbeya baada ya mchezo wao wa kwanza na timu ya jiji ya Mbeya City ambao uliwapa Azam FC faida ya pointi tatu muhimu baada ya kushinda goli 3 dhidi ya wenyeji wao Mbeya City. 

Kuelekea mchezo huo wa siku ya jumatano, kocha mkuu wa timu ya Azam FC Stewart John Hall ametamba kwamba timu yake imejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi zote sita kwa kuwapiga Tanzania Prisons katika uwanja wao wa nyumbani.

 Upande wa wenyeji wa Azam FC, Tanzania Prisons ambao wamewasili mkoani Mbeya jana wakitokea huko mkoani Tanga waliko toa suluhu ya 1-1 na timu ya JKT Mgambo , kocha wa Tanzania Prisons Salum Mayanga wamesema kuwa kutokana na uchovu wa safari wanaendelea na mazoezi ya kawaida ila watahakikisha kuwa wanashinda mchezo huo . 

Tanzania Prisons na Azam FC wanaingia mchezoni jumatano ya keshokutwa wakati Tanzania Prisons wakishikilia nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi jumla ya 31 wakiwa wamecheza michezo 19 na wakati huo wao Azam FC wanashikilia nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi wakiwa na jumla ya pointi 45 huku wakiwa wamecheza michezo 18 katika ligi kuu soka Tanzania Bara

0 Responses to “AZAM NA PRISONS ZAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA MCHEZO WA LIGI KUU JUMATANO MBEYA”

Post a Comment

More to Read