Sunday, February 21, 2016
ISIS WAMCHINJA KIJANA KWA KUSIKILIZA MUSIKI WA POP
Do you like this story?
KUNDI la wapiganaji la ISIS limemuua kwa
kumkata kichwa kijana mmoja baada ya kumkuta akisikiliza muziki wa Pop
unaoimbwa na wasanii wa Marekani akiwa kwenye baa ya baba yake.
Kijana huyo, Ayham Hussein (15) alikamatwa
mjini Mosul, Iraq baada ya wapiganaji waliokuwa kwenye doria kumsikia
akisikiliza muziki huo.
Mauaji hayo yalifanyika nje ya msikiti baada
ya Hussein kutiwa hatiani na mwili wake umekabidhiwa kwa wazazi wake kwa
taratibu za mazishi.
Mbali na kuuawa Hussein, vijana wengine
wawili nao wameuawa kwa kupigwa risasi nje ya msikiti kwa kutohudhuria Swala ya
Ijumaa.
ISIS walipiga marufuku miziki ya nchi za
magharibi kupigwa kwenye maeneo yao huku sababu kuu ikitajwa kuwa miziki hiyo
ni chanzo cha vitendo viovu, majaribu pamoja na kumfanya mtu kushindwa
kujifunza Koran hivyo kumsahau Mungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ISIS WAMCHINJA KIJANA KWA KUSIKILIZA MUSIKI WA POP”
Post a Comment