Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi na wafanyakazi wa Nmb..(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
Benki
ya NMB imezindua kituo cha biashara (NMB BUSSINESS CENTER) katika mkoa wa Mbeya
kitakachokuwa kikiinua na kuboresha uendeshaji wa biashara kwa wafanya biashara
katika mkoa huo.
Akiongea
na fahari News mkurugenzi wa wateja wa NMB Tanzania Abdulmajid Nsekela amesema
kuwa lengo la vituo vya biashara kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ni
kufanikisha kufanya shughuli zao na kupata elimu bora ya kifedha na wanataraji
kuendelea kuwafikia wafanyabiashara popote walipo kwa huduma bora.
Aidha
mkurugenzi huyo wa wateja ameeleza kuwa katika mpango huo wanataraji
kufanikisha malengo ya wateja wao ambao ni wafanyabiasha wakubwa , wakati ,
wadogo sambamba na wakulima kwa kuboresha biashara ya kilimo.
Pia Nsekela
amefahamisha kuwa pamoja na kufanya shughuli za kibenki pia wanachangia
shughuli za kijamii katika kuchangia maendeleo na wanatenga pato lao la mwaka
kwa kuchangia sekta ya afya na elimu ikiwa na lengo la kuiunga mkono serikali
ambapo wanatenga asilimia moja katika pato la mwaka kufanya shughuli hizo.
Mkurugenzi
huyo wa wateja kwenye benki ya NMB Tanzania amewataka wateja wa kati
kuchangamkia fursa hiyo ambayo inawapa nafasi wafanya biashara kupanda kutoka
daraja moja kwenda lingine kulingana na ufanisi wa vituo vya biashara na elimu
ya kifedha watakayopatiwa na NMB.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha biashara cha NMB mkoa wa Mbeya
ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya
Abbas Kandoro amewataka wafanyabiasha na wakazi wa mkoa huo kuitumia fursa za
kibenki ambazo zinatolewa ili kufikia malengo yao ya kibiashara.
Kandoro
amefahamisha kuwa kabla ya kuchukua mkopo wanatakiwa kufanya tathimini na kujua
biashara gani ambayo wanaweza kufanya na kuweza kurejesha marejesho ya benki.
Pia
Kandoro aliwataka viongozi wa benki ya NMB kuangalia suala la riba katika
mikopo wanayotoa kwa vile wananchi wengi wanaogopa kukopa kutokana na baadhi ya
mabenki nchini kutoza riba kubwa jambo linalowawia vigumu wafanyabiasha wadogo
kujenga kasumba ya kuhofia mikopo kwa ajili yakujiendeleza kichumi na kupanua
wigo wa biashara zao.
Benki
ya NMB pia imejikita kwenye shughuli za kilimo kwa kuwezesha urahisi wa
upatikanaji wa pembejeo ambapo hivi karibuni wameanzisha mpango wa kuwapatia
wateja wake matrekta kwa bei rahisi baada ya kuingia mkataba na kampuni ya
Jebiz ambao ni wasambazaji wa matrekta
Pia
NMB inamatawi 175 ATM zaidi ya 600 mawakala ambao wanarahisisha shughuli za
kibenki zaidi ya 450 na wamejiunga na mitandao ya kifedha ya makampuni ya simu
yote
Kwa
upande wa mikopo mkuu wa kitengo cha biashara James Meitaron ameeleza utaratibu
mzima wa utoaji wa mikopo kiwango ambacho wanaanzia kutoa mikopo kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni
thelathini(milioni 30) mkopo ambao unapatikana ndani ya siku mbili ambapo benki
hiyo imempa mamlaka meneja wa tawi kufanikisha mikopo ya kiwango hicho.
kama
biashara yako imeanza kukua kituo cha biashara ambapo kwa mbeya kipo NMB
Mwanjelwa wanatoa mkopo kuanzia milioni 30 mpaka bilioni 2.
Amesema Meitaron kuwa riba ya mikopo kwa benk hiyo haizidi
asilimia 23 kwa mwaka na kadri unavyolipa mkopo riba inapungua mpaka kufikia
asilimia 18 kulingana na mkopo uliokopa.
|
0 Responses to “BENKI YA NMB MBEYA YAZINDUA KITUO CHA BIASHARA (NMB BUSINESS CENTER) MBEYA.”
Post a Comment