Saturday, February 20, 2016
PLUIJM AWAPANGIA SIMBA MABEKI WATATU KATIKATI, NI BOSSOU, TWITE NA NGONYANI
Do you like this story?
KOCHA
Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ameanzisha mabeki watatu wa kati kwa
ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu Simba SC
jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pluijm amewaanzisha kwa pamoja kucheza katikati Mtogo Vincent Bossou, Mkongo Mbuyu Twite na mzalendo Pato Ngonyani.
Langoni yupo Ally Mustafa ‘Barthez’, beki wa kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, wakati viungo ni Thabani Kamusoko, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima na washambuliaji ni Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
Kikosi
cha Yanga SC kinachoanza leo; Ally Mustafa ‘Barthez’ Juma Abdul, Vincent
Bossou, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Deus Kaseke, Thabani
Kamusoko, Amissi Tambwe Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Mwashiuya, Simon Msuva, Malimi Busungu na Issoufou Boubacar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PLUIJM AWAPANGIA SIMBA MABEKI WATATU KATIKATI, NI BOSSOU, TWITE NA NGONYANI”
Post a Comment