Saturday, April 30, 2016
WAFANYABIASHARA WALIOFICHA SUKARI DWAANZA KUKAMATWA
Do you like this story?
Kauli
ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameficha
sukari ili kutengeneza uhaba sokoni utakaopandisha bei ya bidhaa hiyo,
imedhihirika baada ya baadhi ya wafanyabiashara hao kuanza kukamatwa wakiwa na
vidhibiti.
Kutokana
na hali hiyo iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo kuanza kupanda, Waziri Mkuu
Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali kuagiza sukari yake nje itakayouzwa kwa
bei elekezi kwa wananchi ya Sh 1,800 kwa kilo, ili kuzuia ongezeko hilo haramu
la bei.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi alitangaza
polisi kuwashikilia wafanyabiashara wawili wa mjini hapa kwa tuhuma za kukutwa
na zaidi ya mifuko 655 ya sukari, sawa na tani 24.3, ikiwa imekifichwa kwenye
stoo zao.
Kwa mujibu
wa Amanzi, wafanyabiashara hao walikamatwa kwenye msako ulioendeshwa na
watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Singida pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya.
Amanzi
alisema kuwa msako huo uliendeshwa baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna
baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameficha sukari, ili waje kuiuza kwa bei
ya juu kwa wateja wao kwa kisingizio kuwa kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.
“Katika
msako huo, tumemnasa Mohamed Alute Ally (44), mfanyabiashara wa eneo la
Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman
(39), mfanyabiashara wa eneo la Minga katika manispaa ya Singida aliyepatikana
na mifuko 320 ya kilo 50,” alisema.
Mkuu huyo
wa wilaya ametoa mwito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuficha bidhaa zote
muhimu, ikiwemo sukari na mchele, bali waiuze kwa bei halali kwa wateja wao.
Wakati huo
huo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Mchina, amesema msako mkali
unaohusisha kikosi kazi maalumu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama
utaendelea kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa kuhodhi bidhaa kwa sababu yoyote
ile ni kosa la uhujumu uchumi.
Mmoja wa
Wakala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mjini, Salim Nagji, amesema mfuko
mmoja wa sukari huuzwa Sh 92,650 lakini tangu sukari iadimike mfuko unauzwa
kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na Sh
2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya Sh 1,800.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAFANYABIASHARA WALIOFICHA SUKARI DWAANZA KUKAMATWA”
Post a Comment