Saturday, April 30, 2016
TCRA YATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA WANAOBADILI IMEI ZA SIMU FEKI ILI KUWAHADAA WANANCHI
Do you like this story?
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa wafanyabiashara wa vifaa vya
mawasiliano, kuacha kuwahadaa wananchi kwa kutoa punguzo ili kuwashawishi
kununua simu bandia na kutishia kuwafunga miaka 10 jela, faini ya Sh30 milioni
au vyote kwa pamoja watakaobainika.
Hatua hiyo
imekuja wakati mamlaka hiyo ikiwa katika hatua ya kutekeleza mfumo wa rajisi ya
namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi, huku ikitarajia
kuzima simu feki ifikapo Juni 16.
Akizungumza
na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Mhandisi James
Kiraba alisema kuna wafanyabiashara wajanja wanaobadilisha namba za utambulisho
za vifaa vya elektroniki (IMEI) ili kuwahadaa wateja kuwa simu zao siyo feki.
Kwa ujanja
huo, namba ya utambulisho inakuwa inatumika na simu zaidi ya moja na
kutambulika na mfumo licha ya kuwa ni feki.
Pamoja na
kuonekana ni halisi kwa kipindi wanachozinunua, alisema simu hizo
zinazobadilishwa IMEI nazo zitazimwa Juni 16 kwa kuwa ni feki.
“Mamlaka
inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kuwa ni kosa
kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mikononi (mobile devices),
kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 au faini isiyopungua Sh30
milioni au vyote kwa pamoja,”alisema.
Alisema
kumekuwa na udanganyifu kwa baadhi ya wauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa
wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu.
Kiraba
alisema wananchi wanapaswa kuwa makini na hilo, huku wakihakikisha kuwa simu
zao zimehakikiwa ili kuzuia usumbufu wa aina yoyote, utakaoweza kujitokeza
wakati kipindi cha mpito kitakapomalizika.
Alisema
idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zimeendelea
kupungua kutoka asilimia 30 Desemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 13 Machi.
Alisema
uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa
hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu, vilevile idadi ya namba
tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 huku simu halisi
zilikuwa sawa na asilimia 79.
“Uchambuzi
wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa
sawa na asilimia nne, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa
zilikuwa sawa na asilimia 13, uchambuzi huu unahusisha makampuni yote ya simu
nchini,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TCRA YATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA WANAOBADILI IMEI ZA SIMU FEKI ILI KUWAHADAA WANANCHI”
Post a Comment