Thursday, August 18, 2016
WAZIRI MKUU AWAWEKA SAWA WATUMISHI WA OFISI YAKE, TAYARI KWA SAFARI YA DODOMA
Do you like this story?
Waziri
Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.
Ametoa
kauli hiyo leo Agosti 18, 2016 alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi
yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amewataka watumishi hao watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni
utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo
lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.
“Tangu
wakati huo kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuandaa miundombinu
na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu
hiyo,” amesema.
“Pia
tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23,
2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25,
kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka
msisitizo,” amesema.
“Napenda
kuwatoa hofu, mambo yanaenda vizuri ila mtambue kuwa safari imeiva sasa.
Kikubwa ni kwamba tutakwenda kwa awamu kama ambavyo imepangwa,” amesema.
Amewataka
watumishi hao wazidishe mshikamano miongoni mwao huku wakitambua kuwa wana
dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na uaminifu.
“Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu tunapaswa tutambue dhamana tuliyonayo. Tufanye kazi kwa
bidii. Tuhakikishe kila kilichopangwa kinafanyika kwa ufanisi na kinafanikiwa,”
amesema.
Julai
25 katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Waziri Mkuu aliwataka mawaziri wote
kuhamia Dodoma mara moja na kusema kuwa yeye atakuwa wa kwanza ifikapo
Septemba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ WAZIRI MKUU AWAWEKA SAWA WATUMISHI WA OFISI YAKE, TAYARI KWA SAFARI YA DODOMA”
Post a Comment