Thursday, August 11, 2016
ZAMBIA WAPIGA KURA YA URAIS NA WABUNGE LEO
Do you like this story?
Leo Zambia inaingia kwenye historia
ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa kumchagua
Rais wa Nchi pamoja na wabunge
watakaoenda kuiongoza Serikali hiyo kwa awamu nyingine.
Ukuaji wa demokrasia unaonekana kukua
kwa kasi barani Afrika, baada ya kuwepo kwa upinzani mkali katika baadhi ya chaguzi barani hapa,
hali hii imeonekana tena Nchini Zambia baada ya kuwepo kwa upinzani mkubwa
katika kipindi cha kampeni huku vyama viwili vya Siasa kati ya PF chini ya
mgombea wake Edgal Lungu ambae ndie Rais kwa sasa na wapinzani wao UPND chini
ya mgombea wake Hakainde Hichilema.
Katika kipindi cha kampeni
kuriripotiwa kutokea kwa vurugu za kisiasa katika baadhi ya maeneo Nchini
Zambia, leo Wananchi hao wanatimiza haiki yao ya kupiga kura kwa ajili ya
kumchagua Rais pamoja na wawakilishi wao (wabunge).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “ZAMBIA WAPIGA KURA YA URAIS NA WABUNGE LEO”
Post a Comment