Wednesday, November 2, 2016
BUNDUKI 11 ZA UJANGILI ZAKUTWA NYUMBANI KWA MBUNGE.
Do you like this story?
Kasi
ya kupambana na ujangili iliyoongezwa na Rais John Magufuli imeendelea kuzaa
matunda huku Kikosi Kazi Maalum kilichoundwa kikiripotiwa kukamata bunduki 11
nyumbani kwa mbunge.
Kwa
mujibu wa chanzo cha gazeti la Mwananchi, Bunduki hizo zinazosadikika kutumika
katika matukio ya ujangili zilikutwa nyumbani kwa mbunge wa CCM ambaye jina
lake limehifadhiwa kwa sababu za kutoingilia unyeti wa oparesheni hiyo.
Taarifa
hizo zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya
kushtukiza katika Ofisi za Maliasili na Utalii na kukipa nguvu zaidi kikosi
kazi hicho ambacho kilidaiwa kuanza kuzimwa.
Rais
Magufuli alimtaja mtu mmoja kwa jina la ’Mpemba’ anayehusishwa na biashara
haramu ya pembe za ndovu kwa muda mrefu na kueleza kuwa angeshangaa kama
asingekamatwa. Alishuhudia meno 50 ya Tembo ambayo yalikamatwa kutokana na
oparesheni hiyo, hali inayoonesha kuna tembo 25 waliuawa.
Naye
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe juzi alieleza kuwa
tayari wameshamtia nguvuni Mpemba na kwamba wanaendelea na msako wa wengine
ambao wakikamatwa nchi itatikisika kutokana na majina yao.
”Hilo
ni jina lake analolitumia katika harakati zake za biashara ya ujangili ili asitambulike.
Yuko mwingine pia anajiita ’Mangi wa Kabila fulani’ lakini sio majina yao
halisi,” alisema Profesa
Maghembe na kuongeza kuwa hawaweki hadharani majina yao ili kutoharibu
uchunguzi.
Profesa
Maghembe aliwahakikishia Watanzania kuwa mtandao wote wa majangili utavurugwa
na hakuna jangili atakayesalimika bila kujali jina lake.
Hivi
karibuni, Rais Magufuli alimteua Mkuu wa Majeshi wa zamani, Jenerali George
Waitara kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), ambaye
ameahidi kuwakomesha wafanyabiashara hao haramu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BUNDUKI 11 ZA UJANGILI ZAKUTWA NYUMBANI KWA MBUNGE. ”
Post a Comment