Tuesday, April 18, 2017
Mbunge wa Chadema Alazwa Ghafla Muhimbili, Afanyiwa Upasuaji
Do you like this story?
Wakuu
salaam. Natumai tupo wazima. Kama inavyozunguka mitandaoni kuhusu
kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Mhe. John Heche, taarifa
hiyo ni ya kweli.
Mhe.
Heche alifika Hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya Jumanne wiki hii kwa
uchunguzi wa afya yake, baada ya uchunguzi wa awali alishauriana na
daktari wake na kukubaliana angerejea Hospitali baada ya wiki mbili kwa
matibabu rasmi.
Hata
hivyo jana usiku Mhe. Heche alipata maumivu makali ya ghafla tumboni na
leo asubuhi alikimbizwa Hospitali Muhimbili na kufanyiwa upasuaji
(specialised surgery).
Upasuaji umeenda vizuri na hali yake inaendelea vema sana. Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe amemtembelea kumjulia hali.
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
CHADEMA
Jumapili April 16, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)