Friday, May 19, 2017

Mwanamke akutwa na kete 208 za dawa za kulevya


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Pili Majaliwa Khamis (Bi. Kei) mwenye umri wa miaka 38 amekutwa na kete 208 zinazoaminika kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroin nyumbani kwake.
Awali, Jeshi la polisi lilimtia mbaroni kijana Omar S. Omar mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Bububu wilaya ya Magharibi A akiwa anasambaza unga huo na ndipo alipomtaja Bi. Kei kama mmiliki wa unga huo, hata hivyo mwanamke huyo alikimbia makazi yake hayo.
Kamadna wa polisi mkoa wa Mjini magharibi Hassan Nassir Ali amesema “Mapambano haya yanayofanywa katika wilaya zetu za mjini magharibi dhidi ya madawa ya kulevya, ni mapambano endelevu”
Aidha kamanda huyo ameiomba jamii kutoa mashirikiano kwa jeshi la polisi ili kutokomeza vitendo hivi vinavyofanywa na baadhi ya watu.

0 Responses to “Mwanamke akutwa na kete 208 za dawa za kulevya ”

Post a Comment

More to Read