Thursday, June 1, 2017

UEFA CHAMPIONZ LIGI: FAINALI JUMAMOSI JUVE NA REAL, TIMU ZILIZOPAMBANA MARA 18 ULAYA!


>PATA UNDANI:
Juventus na Real Madrid zitakutana kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumamosi Juni 3 huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales na hiyo itakuwa mara yao ya 19 kucheza kwenye Mashindano haya ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kila Timu imeshinda mara 8 na Sare 2 Juve ikifunga Bao 21 na Real 18.
PATA NINI KILIJIRI KATIKA MARA HIZO 18:
1961/62 Robo Fainali Kombe la Klabu Bingwa Ulaya
Juventus 0-1 Real Madrid
Real Madrid 0-1 Juventus
Real Madrid 3-1 Juventus (Marudiano Paris, France)
1986/87 Raundi ya Pili Kombe la Klabu Bingwa Ulaya
Real Madrid 1-0 Juventus
Juventus 1-0 Real Madrid (Baafa Dakika za Nyongeza, Real Madrid walishinda kwa Penati 3-1)


1995/96 Robo Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI
Real Madrid 1-0 Juventus
Juventus 2-0 Real Madrid
-Real walishinda Mechi ya Kwanza kwa Bao la Raúl González.
Kwenye Mechi ya Pili Juve waliibuka kidedea kwa Bao za Alessandro Del Piero na Michele Padovano.
1997/98 Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI
Juventus 0-1 Real Madrid
-Fainali hii ilichezwa huko Amsterdam ArenA, Nchini Netherlands na Predrag Mijatović kuwapa Real Bao pekee na la ushindi Dakika ya 66.
2002/03 Nusu Fainali UEFA CHAMPIONZ LIGI
Real Madrid 2-1 Juventus
Juventus 3-1 Real Madrid
-Real walishinda Mechi ya Kwanza kwa Bao za Ronaldo na Roberto Carlos huku Juve wakifunga Bao lao pekee kupitia David Trezeguet.
Katika Mechi ya Pili, Juve walipiga Bao 3 kupitia Trezeguet, Del Piero na Pavel Nedvěd wakati Real wakifunga Bao lao 1 kupitia Zinédine Zidane.
2004/05 Raundi ya Mtoano ya Timu 16 UEFA CHAMPIONZ LIGI
Real Madrid 1-0 Juventus
Juventus 2-0 Real Madrid (Baada Dakika 120)
-Juve walifungwa Mechi ya Kwanza huko Madrid 1-0 kwa Bao la Iván Helguera lakini katika Mechi ya Pili huko Turin Trezeguet aliipa Bao zikibaki Dakika 15 na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30 Marcelo Zalayeta akapiga Bao la Pili na la ushindi kwa Juve katika Dakika ya 116 kwenye Mechi ambayo Ronaldo na Mchezaji wa Juve kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 113.
2008/09 UEFA CHAMPIONZ LIGI Makundi
Juventus 2-1 Real Madrid
Real Madrid 0-2 Juventus
-Juve walishinda Mechi zote 2 za Makundi na Mechi ya Kwanza Bao za Juve zilifungwa na Del Piero na Amauri na la Real kupachikwa na Ruud van Nistelrooy wakati Mechi ya Pili Del Piero alipiga Bao zote mbili.
Timu hizi 2 zilifuzu kutoka Makundi lakini zilikwama Hatua ya iliyofuatia.
2013/14 UEFA CHAMPIONZ LIGI Makundi
Real Madrid 2-1 Juventus
Juventus 2-2 Real Madrid
-Safari hii Real waliwanyosha Juve kwenye Makundi kwa Bao 2 za Cristiano Ronaldo katika Mechi ya Kwanza huku Fernando Llorente akiwapa Juve Bao lao 1.
Mechi ya Pili ngoma ilikuwa Sare kwa Bao za Arturo Vidal na Llorente na Real kupiga kupitia Ronaldo na Gareth Bale.
2014/15 UEFA CHAMPIONZ LIGI Nusu Fainali
Juventus 2-1 Real Madrid
Real Madrid 1-1 Juventus
-Wakikutana kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2002/03, Juve waliwalaza Real kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa Nyumbani kwa Bao za Álvaro Morata na Carlos Tévez wakati Bao la Real likipigwa na Ronaldo na kutoka Sare huko Madrid wakifunga Bao lao moja kupitia Alvaro Morata zikisalia Dakika 12 wakati Ronaldo aliwafungia Real kwa Penati Dakika ya 23 na kuwapa matumaini ya kusonga.
**Juventus wamekuwa Mabingwa wa Ulaya mara 2, Real Madrid wao wamebeba Kombe mara 11.

0 Responses to “UEFA CHAMPIONZ LIGI: FAINALI JUMAMOSI JUVE NA REAL, TIMU ZILIZOPAMBANA MARA 18 ULAYA!”

Post a Comment

More to Read