Friday, July 28, 2017
WAZIRI MHAGAMA AWASHA MOTO MBEYA , AWAPA SIKU 30 WAAJIRI WOTE NCHINI KUJISAJILI WCF
Do you like this story?
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza leo Julai 27, 2017 wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa kushtukiza kwenye Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati jijini Mbeya ili kubaini kama mwajiri kwenye hospitali hiyo amejisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF).
Waziri ametoa siku 30 kwa waajiri kutoka sekta ya
umma na binafsi Tanzania Bara, kujisajili na Mfuko huo, vinginevyo watakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo faini ya shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdusalaam Omar.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini
ambao hawajasajili, kujisajili katika
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa michango kwa wakati, vinginevyo hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri
Mhagama alitoa agizo hilo jijini Mbeya Julai 27, 2017 wakati wa zoezi
la ukaguzi wa kushtukiza jijinihumo kuwabaini waajiri ambao bado
hawajatekeleza Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka
waajiri wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara kujisajili kwenye
Mfuko huo.
“Mwajiri
ambaye hajajisajili kwenye Mfuko,anaweza kufikishwa mahakamani na
adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi chafedha kisichozidi shilingi
milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5 jela auvyote kwa pamoja,
hivyo nawasihi waajiri kutoka sekta binafsi na umma Tanzania Bara ambao
hawajasajili kutekeleza sheria hiyo inayowataka kujisajili WCF katika
muda huo nilioutoa.” Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Katika
ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mhe. Waziri alifuatana na
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba naTathmini wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge na Afisa Kazi wa Mkoa
wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya ambapo taasisi ya kwanza ambayo Mhe. Mhagama
aliikagua
ni Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na St. Aggrey iliyoko Uyole
na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika Mfuko.
Aidha
Waziri alitoa siku saba kwa waajiri wote Mkoani Mbeya wapatao 107 ambao
bado hawajajisajili ikiwemo Hospitali ya K’s na Shule ya sekondari St.
Aggrey kujisajili ndani ya muda huo.
“Mkishindwa
kutekeleza agizo hilo maana yake mnatuelekeza kutumia kifungu cha
71(4), cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kinachotamka adhabu ya faini
ya kiasi cha fedha kisichopungua
shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja.” Alisema.
Aidha
Waziri Jenista alihimiza kuwa mwajiri anapojisajili na Mfuko pia
atimize wajibu wa kisheria wa kuchangia katika Mfuko kwa wakati stahiki.
Mhe. Waziri alisema nia ya Serikali ya awamu
ya
Tano sio kuwatisha waajiri bali ni kuhakikisha wanafuata sheria ili
hatimaye, wafanyakazi wapate haki yao stahiki pindi wanapoumia, kuugua
ama kufariki wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri wao kwa
mujibu wa mkataba wa ajira.
Akifafanua
zaidi Waziri alisema, takwimu zilizopo katika Mfuko za kipindi cha
mwaka 2015/16 na 2016/17zinaonesha kuna jumla ya waajiri 229 jijini
Mbeya na kati yao ni waajiri 107 tu ndiyo waliojisajili katika Mfuko.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa WCF, Dk.
Abdulsalaam Omar alisema Mfuko unamshukuru Mhe. Waziri kwa kushiriki
katika ukaguzi huu wa kwanza wa aina yake
kufanyika tangu Mfuko huu uanzishwe mnamo mwaka 2015 na kwamba Mfuko utasimamia
na kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri.
"Kwa
kipindi chote hicho Mfuko umekuwa ukijikita zaidi katika kutoa elimu
kwa wadau mbalimbali wakiwemowaajiri ili waweze kuelewa umuhimu wa
kujisajili katika Mfuko na faida ambazo
mwajiri
na mfanyakazi atazipata pindi anapoumia, kuugua au kufariki wakati
akitekeleza majukumu ya mwajiri,” alisisitiza Dkt Omar.
Akifafanua
zaidi, Mkurugenzi huyo alisema katika kazi ya uelimishaji kwa kipindi
cha mwaka 2016/2017 Mfuko ulitoa elimukwa waajiri wapatao 4,901 kuhusu
haki na wajibu lakini pia kuelewa sheriakuhusu wajibu wa waajiri
kujisajili katika Mfuko. Aidha Mfuko umekuwa ukitumia
njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari, semina lakini pia kwa kuwaandikia
waajiri kuhusu umuhimu wa wao kutekeleza sheria hiyo kwa kujisajili katika
Mfuko na kutoa Michango kwa wakati kama ambavyo sheria inaelekeza.
Dkt
Omar alisema Mfuko ulianza kutekelezamajukumu yake tarehe 1 Julai 2015
kama ilivyoelekezwa katika tangazo la Serikali Na. 169/2015 ambapo
majukumu hayo ni pamoja na kusajili waajiri, kukusanya michango na
kulipa fidia stahiki.
Tayari Mfuko umeanza kulipa fidia kwawafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kuanzia tarehe 1 Julai 2016.
Ili
mfanyakazi aweze kulipwa fidia, nilazima mwajiri wake awe amechangia
katika Mfuko, hivyo waajiri wanao wajibu kisheria chini ya Vifungu vya
71 – 78 vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
kujisajili, kuwasilisha michango, kutoa taarifa ya matukio ya ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi pamoja na kuwasilisha mapato ya mwaka." Alifafanua Dkt.
Omar.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura
Kunenge alisema, "Tamko alilotoa Mhe. Waziri wetu litakuwa chachu kwa
waajiri wengine nchini kujiunga na Mfuko kwa kujisajili na kuwasilisha
michango kwa wakati na hivyo kuwezesha kufikia lengo la Mfuko la kulipa
Fidia Stahiki kwa wakati",alisema.
Bi.
Kunenge pia alisema, Ofisi za WCF ziko wazi na kwamba huduma za Mfuko
huo zinapatikana kila mkoa hapa Tanzania Bara ambapo Maafisa Kazi wa
Mikoa ndio wanafanya kazi kwa niaba ya Mfuko kwa sasa.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), na
Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya, (kulia), wakiuliza
alipo mkurugenzi wa Hospitali ya K's mara baada ya kuwasili na waziri
Mhagama katika ziara ya ukaguzi wa kushtukiza leo Julai 27, 2017.
Waziri
Mhagama, (wakwanza kulia), Bi. Laura na Dkt. Omar, wakimsubiri
Mfanyakazi huyu wa K's Hospital akiwasiliana kwa simu na mwajiri wake
ili kumjulisha uwepo wa Waziri na ujumbe wake kwenye hospitali hiyo.
Maafisa wa polisi wakiwa tayari kuhakikisha usalama unazingatiwa wakati wa zoezi hilo.
Waziri Mhagama na Dkt. Omar(kushoto), wakisubiri ujio wa Mkurugenzi wa hospitali ya K's
Afisa
Matekeelzo Mwandamizi wa WCF, Bw.Dan Kapogo, (kulia), akijadiliana
jambo na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto),
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Dan Kapogo,na Afisa Kazi
Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya, wakijadiliana jambo.
Mhe.
Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Hospitali ya K's Dkt.Victoria
Kanama, baada ya kuitwa ili aonane na waziri kueleza kwa nini
hajajisajili na Mfuko licha ya kupatiwa elimu lakini pia kujulishwa kwa
barua.
Dkt.
Omar, Kulia), akimuongoza waziri Mhagama wakati wakitoka kwenye
Hospitali ya K's baada ya ukaguzi. (wakwazna kushoto) ni Mkurugenzi wa
Hospitali hiyo, Dkt.Victoria Kanama.
Dkt.
Omar akitoa shukrani za WCF kufuatia ziara hiyo ya kushtukiza
aliyofanya Mhe. Waziri na kubainisha kuwa maagizo hayo yatasimamiwa na
kutekelezwa.
Bi. Kunenge na Bw. Kapogo kutoka WCF wakijadiliana jambo
Mratibu wa Hospitali ya K's Bw.Mtunda Mwankwasya akizungumza.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge
Afisa
Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya akizungumza. "Tumewapa
taarifa waajiri wote mkoani Mbeya hivyo wanajua fika kuhusu sheria hii
inayowataka kujisajili na kutoa Michango katika Mfuko.
Dkt. Omar akiteta jambo na Mhe. Waziri Mhagama.
Waziri akitoka kwenye Hospitali ya K's akiongozana na Mratibu wa hospitali hiyo,Bw.Mtunda Mwankwasya
Mkuu wa shule ya St. Aggrey.
Waziri Mhagama akizungumza mbele ya Meneja wa shule ya St. Aggrey, Bw.Melas Paul Mdemu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI MHAGAMA AWASHA MOTO MBEYA , AWAPA SIKU 30 WAAJIRI WOTE NCHINI KUJISAJILI WCF”
Post a Comment