Wednesday, July 26, 2017
Rais Magufuli akamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika mikoa minne
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli leo tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya
siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua
barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.
Barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ina
urefu wa kilometa 89.3 na imejengwa gharama ya Shilingi Bilioni 114.692,
fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza na wananchi wa Itigi katika sherehe za ufunguzi wa
barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth
Magufuli, amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele
kwa kuwa barabara hiyo pamoja na nyingine saba alizozifungua katika
ziara hii zenye urefu wa jumla ya kilometa 707 zimejengwa kwa gharama ya
Shilingi Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya
Tanzania.
Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa
barabara imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali
nchini na kwamba Serikali imeamua kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini
kwa lengo la kuhakikisha barabara za vijijini zinajengwa kwa kiwango
cha lami.
Kwa barabara ya Mkiwa – Itigi yenye urefu wa kilometa 57 na ambayo
tayari zabuni ya ujenzi ilishatolewa kwa mkandarasi ili aijenge kwa
kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 104, Mhe. Rais Magufuli
ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya
mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa kiwango cha fedha
kilichopangwa ni kikubwa ikilinganishwa na gharama halisi.
Pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa Mnyaa kujadiliana na Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili
aweze kuendelea kujenga barabara kutoka Itigi kuelekea Chunya hadi
Makongorosi Mkoani Mbeya.
Pamoja na wananchi wa Itigi Mkoani Singida, Mhe. Dkt. Magufuli
aliyetokea Tabora amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake
katika vijiji vya Kigwa, Kizengi na Tura Wilayani Uyui na amewataka
kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kuzingatia
uzalishaji mazao yanayostahimili ukame kama vile uwele, mtama, viazi na
muhogo ili kuepuka tatizo la upungufu wa chakula.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kuhamasisha
wananchi kufanya kazi hususani shughuli za kilimo ambacho ni uti wa
mgongo wa Taifa, na ameonya kuwa kiongozi ambaye hatatekelezi agizo hilo
atakuwa hafai na ataondolewa.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hamasisheni
watu kufanya kazi na kama kuna viongozi na watendaji wasiotekeleza
wajibu huo katika maeneo yenu waondoeni mara moja” ameagiza Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli katika ziara ya
leo ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Hamis Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu Prof. Norman Sigalla King na Wabunge wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Rais Magufuli amewasili katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia Wananchi Kijiji Cha Tula Uyui Mkoani Tabora waliojitokeza
Barabarani Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea
kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza
jambo akiawa njiani katika moja ya mikutano ya barabarani kwa
waliojitokeza Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea
kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati Rais
alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi
-Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa na Serikali
kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya
siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi
-Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za
Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye
Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya
Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017.
Wananchi
wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa Barabara
ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa
fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea
kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao
Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wapili
kushoto na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida,wakiondoa kitambaa
kuashiria Kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye
urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia
mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu
Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma
Julai 25,2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi
wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora Wakikata Utepe kama ishara ya
kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa
kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia
moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni
Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai
25,2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akiteta jambo na Wang Chao mwakilishi wa Pawer China Internatinal Group
Limited wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye
urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia
mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu
Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma
Julai 25,2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwashukuru na kuwasalimia kwa kupunga mikono kwa wananchi wa Itigi na
Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa Barabara ya Itigi
-Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za
Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye
Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya
Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Rais Magufuli akamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika mikoa minne”
Post a Comment