Tuesday, July 11, 2017
MANTRAC TANZANIA YAZINDUA KUKODISHA NA KUMILIKI MITAMBO
Do you like this story?
Mr Hatem Farouk Managing Director wa Mantrac Tanzania |
Bw Valence Pantaleo Mkuu wa kitengo cha Mipango biashara na Masoko katika kampuni ya Mantrac Tanzania. |
Kampuni ya
Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa
kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua
mtambo kwa mara moja.
Hii
inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac
Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki
kamili wa mtambo huo.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. Alisema
katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia
matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.
Mpango wa
kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara
kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa
kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.
Mpango huu
unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa
mkandarasi au mfanyabiashara.
Kampuni ya
Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya
Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa
inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
Miradi hii
mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo,
madaraja, kwenye madini na kilimo.
Bidhaa
zinazouzwa na kampuni ya Mantrac Tanzania zinapatikana katika matawi mbalimbali
nchini kama vile Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Mbeya, na Kilimanjaro.
Bw Pantaleo
alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara kati ya kampuni ya
Mantrac Tanzania na wateja kwenye mitambo mipya, iliyotumika na kukodisha
mitambo, sasa kampuni imeamua kuleta mpango huu wa kukodisha na kumiliki ambapo
mteja atalipa kidogo kidogo hadi pale atakapomiliki mtambo wake.
Alisema
kamupuni ina mitambo mingi inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 15
kwa ajili ya kutekeleza mpango huu mpya wa kukodisha na kumiliki.
Kampuni ya
Mantrac Tanzania ndio pekee yenye kibali cha kusambaza na kuuza mitambo
mbalimbali inayotengenezwa na kampuni ya CAT hapa nchini Tanzania.
Kampuni pia
ina vituo maalum vya huduma kwa ajili ya matengenezo ya mitambo, ina wataalamu
wa hali ya juu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa ambavyo hutumika katika
kuchunguza tatizo na kutengeneza ubovu unaojitokeza katika mitambo.
Katika
mpango huu, vigezo na masharti vitazingatiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MANTRAC TANZANIA YAZINDUA KUKODISHA NA KUMILIKI MITAMBO”
Post a Comment