Wednesday, September 6, 2017

WAFANYABISHARA SOKO LA SIDO WARUHUSIWA KUENDELEA NA UJENZI


Mkuu Wa Wilaya ya Mbeya Mh,Paul Ntinika akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sido juu ya uanzaji wa ujenzi ndani ya mwezi mmoja


Wafanyabiashara wa soko la Sido wakimsikiliza Mkuu Wa Wilaya ya Mbeya katika mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya sido

Baadhi ya wafanyabiashara wakiuza biashara zao katika soko la sido baada ya mkuu wa wilaya kuruhusu ujenzi kuanza




Wafanyabiashara  wa soko la sido wakianza ujenzi mara baada ya tamko la Mkuu Wa Wilaya kuwaruhusu kujenga katika mpangilio wa umepangwa na jiji 





SERIKALI Mkoani hapa imetoa muda wa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wa soko la Sido jijini Mbeya,kuhakikisha wanakamilisha Ujenzi wa vibanda, ikiwa ni siku saba tangu itangaze kusimamisha kwa muda usiyo julikana kwa kile kilicho elezwa kuwa mchoro wa soko hilo haukudhibitishwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mbali ni kuruhusiwa kuendelea na ujenzi lakini pia Serikali imetangaza kuwa Ujenzi wa soko hilo utafanyika kwa muda wa mwezi Mmoja kuanzia Septemba 6 mwaka huu na baada ya hapo wafanyabiashara wote wataruhusiwa kuanza biashara bila kulipa Ushuru wa soko kwa muda wa miezi sita.
Akitangaza uamuzi huo  mbele ya wafanyabiashara na wahanga wa moto,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, Mkuu Wilaya ya Mbeya Wiliam Paul Ntinika amesema kuwa uamuzi huo umeamliwa na kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa kwa kuzingatia maslahi mapanaa ya wafanyabishara hao na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa mbali na kuzingia maslahi mapana ya taifa lakini pia kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa iliyafanyia kazi na kuyazingatia maombi ya wafanyabiashara hao yaliyowasilishwa na viongozi wao ya kutaka wabaki eneo hilo lakini pia Serikali iharakishe kutoa ramani ili watu waweze kuendelea na Ujenzi.

Aidha Ntinika amewataka wafanyabishara kutoa ushrikiano kwa watalaamu kutoka Idara ya Mipango Miji,Shirika la Umeme Tanesco,Zimamoto ambao wapo kwa ajili kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalumu wakati wote wa Ujenzi wa soko hilo ambalo Agost 15 mwaka huu liliteketea kwa moto.

Hata hivyo Serikali imewaruhusu kuendelea na Ujenzi kwa mara nyingine ikiwa ni siku saba tangu iwatake wafanyabishara kusimama kwa kile kilichokelezwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haikudhibitisha mchoro huo, na  Zuio hilo linakuja ikiwa ni siku chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla afanye Mkutano na kuwaruhusu kuendelea na ujenzi wa vibanda vya kudumu,katika soko hilo.
Naye mwenyekiti wa Jumuhiya ya wafanyabishara mkoa wa Mbeya, Charlers Syonga ameishukuru serikali kwa kusikiliza kilio cha wafanyabiashara na hatimaye kufikia uamuzi kuwaruhusu wafabiashara kuendelea kubaki katika eneo hilo la sido 

Naye Gibons Bukuku  mfanyabiashara katika soko hilo na mwenye Ulemavu wa miguu ambaye ni muhanga wa tukio la Moto ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuwarejesha katika eno hilo huku akitaka Serikali ilisimamie ujenzi kwa kuweka miundombinu rafiki rafiki kwa watu wenye Ulemavu.

0 Responses to “WAFANYABISHARA SOKO LA SIDO WARUHUSIWA KUENDELEA NA UJENZI ”

Post a Comment

More to Read