Friday, March 7, 2014
AJALI YAUWA, MAGARI YAKWAMA KWA SAA TATU DAR – MORO
Do you like this story?
Mtu mmoja amefariki dunia na
wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa uso na lori katika
eneo la bwawani barabara ya chalinze morogoro.
Ajali hiyo ilitokea jana
saa 4:30 asubuhi baada ya basi hilo aina ya Toyota coaster lilokuwa likitokea
dar es salaam kwenda ifakara kugongana na lori la mafuta lililokuwa likitoka
morogoro kuelekea chalinze.
Kamanda wa polisi mkoa wa
pwani. Ulrich matei alimtaja aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni dereva wa
lori, ally Ngoma(62) .
Kamanda matei alisema
majeruhi 14 wa ajali hiyo ni abiria waliokuwa kwenye basi. Alisema wote
walipelekwa katika kituo cha afya chalinze kwa matibabu.
Amesema ajali hiyo
ilitokea baada ya dreva wa basi kujaribu kuyapita magari mengine katika eneo la
sekondari ya bwawani sehemu ambayo ina mwinuko.
Amesema wakati dereva huyo akijaribu kuyapita magari hayo,
alikutana na lori hilo na kugongana uso kwa uso na kusababisha kifo na majeruhi
hao.
Amesema dereva wa basi
hilo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kaunzia sasa kujibu tuhuma
zinazomkabili
Mbali ya kusababisha kifo
na majeruhi hao, ajali hiyo ilisababisha adha kwa waliokuwa wakitumia barabara
hiyo hasa wale wanaosafiri kati ya dar es salaam na morogoro kwani zaidi ya
magari 200 yalikwama kwa zaidi ya saa tatu.
Ajali hiyo imetokea siku
moja baada ya nyingine iliyosababisha vifo vya watu saba baada ya basi dogo la
abiria kugongana na lori katika eneo la chalinze mzee na kujeruhi tisa.
Akizungumzia ajali hiyo ya
juzi, ofisa habari wa hospitali ya tumbi kibaha , Gerald chami alisema majeruhi
sita hali yao wanaendelea vyema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJALI YAUWA, MAGARI YAKWAMA KWA SAA TATU DAR – MORO”
Post a Comment