Saturday, March 8, 2014

KOCHA MKUU WA SIMBA ZDRAVKO LOGARUSIC ASHTAKIWA.



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Bara kumshughulikia Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic kutokana na tabia yake ya kukataa kuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya mechi za timu yake.
 
Katika siku za hivi karibuni, Logarusic amekuwa akikataa kuingia katika chumba maalum cha mahojiano na waandishi wa habari kama ambavyo taratibu za TFF zinavyomtaka.

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, ameliambia gazeti hili kuwa, wameiagiza Bodi ya Ligi ambayo inasimamia Ligi Kuu Bara kumchukulia hatua kocha huyo baada ya kubaini kuwa ni kweli amekuwa akifanya hivyo.

“Siwezi sema ni hatua gani lakini naamini watafanya kama tulivyowaagiza,” amesema Mwesigwa.
 

0 Responses to “KOCHA MKUU WA SIMBA ZDRAVKO LOGARUSIC ASHTAKIWA.”

Post a Comment

More to Read