Saturday, March 8, 2014
MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA CHANGAMOTO TERE KWA AKINA MAMA WAJANE MBEYA.
Do you like this story?
|
Hii ni nyumba ya mama mjane ambayo aliachiwa ma mumewe ambaye alifariki kwa ajari ya pikipiki. |
|
Mama mjane akiwa na watoto wake mapacha
ambapo alionyesha kububujikwa na machozi kutokana na majonzi ya kufiwa na
muwewe pamoja na mzigo alio nao
|
Licha wanawake Duniani Kote wakiwa katika kusherekea siku yao ambayo imeadhimishwa Machi 8 mwaka huu bado idadi kubwa ya wanawake mkoani mbeya wameendelea kuishi katika mazingira magumu mara baada ya waume zao kufariki dunia kutokana na sababu mbalimbali na kuwa acha wakiwa wajane.
Katika
tukio la kusikitisha Mkazi wa Inyala Kata ya Iyunga jijini Mbeya Bi.Sharifa
Adam( 31) ambaye ni mama mjane mwenye watoto watano amejikuta katika hali ngumu
ya kimaisha kufuatia mume wake kufariki dunia Februali 27 mwaka huu .
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa mama huyo amedai kuwa amekuwa akiishi katika mazingira
magumu mara baada ya mume wake kufariki dunia na kumuachia mzigo mkubwa wa watoto
watano huku yeye akiwa hana shughuli yoyote inayo muingiizia kipato.
Amesema
mume wake alikuwa akijishughulisha na kazi ya Bodaboda katika kituo cha Iyunga
ambapo katika hali ya kusikitisha mumewe huyo aliuwawa na kundi la watu
mara baada ya kumkodisha.
Amesema
mara baada ya kupokea taarifa za kuuwawa kwa mumewe alichukua jukumu la kutoa
taarifa katika kituo cha polisi Iyunga na kwa ndugu wa marehemu ambapo
ulianza msako kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na bodaboda wenzake ambapo
walifanikiwa kuukuta mwili wa mume wake ukiwa umetelekezwa katika kijiji
kimoja wilayani Mbozi.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mama huyo amedai kuwa mara baada ya jeshi la polisi
kufanikiwa kuupata mwiii huo baadae pia pikipiki ya mume wake na watuhumiwa
wote walitiwa mbaroni ambao kwa sasa kesi hiyo ipo kituo cha polisi kwa ajili
ya upelelezi.
Mama
huyo amesema wakati mume wake anafariki alimuachia watoto watano ambao kati yao
watatu walikuwa wakisoma shule ya msingi Ikuti darasa la kwanza na la pili huku
wawili wakiwa wachanga ambao ni mapacha hivyo maisha yake kwa sasa ni magumu
sana na anahitaji msaada wa haraka vinginevyo atawapoteza watoto wake kutokana
na tatizo la njaa.
Hata
hivyo amedai kuwa marehemu mume wake alimuachia nyumba yenye vyumba
viwili ambayo bado hijakamilika hivyo kumfanya aendelee kuishi ndani ya
nyumba hiyo huku ikiwa haina madirisha na watato wake watano.
Kufuatia
hali amewaomba wasamalia wema kujitokeza na kumsaidia mama huyo ambapo pia
watoto wake waweze kwenda shule pamoja na mapacha hao kupata lishe bora.
Hata
hivyo amelitaka Dawati la jinsia la wanawake na watoto mkoani humo kuhakikisha
wanamsaidia kwa haraka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo hatimaye mahakamani
na kutolewa kwa hukumu ili aweze kupata haki yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA CHANGAMOTO TERE KWA AKINA MAMA WAJANE MBEYA.”
Post a Comment