Wednesday, March 19, 2014

RAIS ZUMA ALIFUJA PESA ZA UMMA?.




Mkuu wa idara ya kupokea malalamishi ya umma, Bi Thuli Madonsela hivi leo anatarajiwa kutoa ripoti ya idara hiyo kuhusu uchunguzi wa iwapo Rais Jacob Zuma alihusika katika ufisadi.
Rais huyo wa Afrika Kusini inadaiwa alitumia pesa za umma dola milioni ishirini kukarabati boma lake la kifahari lililopo katika kijiji cha Nkandla alikozaliwa.

Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vimedokeza kuwa Rais Jacob Zuma amefanya mashauriano na Bi Madonzela, hivi karibuni wakati ambapo chama tawala cha ANC kimetoa wito kwa wanachama wake kupuuza repoti hiyo ya Bi Madonzela iwapo itamshirikisha Rais Zuma.

Boma la Nkandla la kibinafsi la Rais Zuma lina nyumba kadhaa, na limewekwa mitambo ya kisasa ya kiusalama ili kumlinda Rais.
Kulingana na mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa, Waziri wa Ujenzi wa Kazi za Umma nchini humo Nthula Tsinthesi, ilikuwa muhimu kukarabati boma hilo kwa kiasi hicho cha pesa kwa sababu boma hilo limewahi kuvamiwa mara tatu na wahalifu.

Ukarabati huo wa boma la Rais ambao sasa umenukia kuwa kashfa umewafanya wengi kuhoji iwapo bwawa la kuogelea la kisasa lililojengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa ni sehemu ya usalama unaotajwa.

Na pia kumekuwepo na habari zinazodaiwa kuwa katika ripoti hiyo ambazo zinadai kuwa Rais Zuma mwenyewe alitoaamri pesa za umma kutumiwa,

0 Responses to “RAIS ZUMA ALIFUJA PESA ZA UMMA?.”

Post a Comment

More to Read