Wednesday, March 19, 2014

WARIOBA AWAKUNA WASOMI, WACHAMBUZI.




baadhi ya wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini wamesema  hotuma ya mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji joseph warioba itasaidia kubadilisha msimamo wa wajumbe wengi  wa bunge maalumu la katiba.

Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya jaji warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba katika bunge hilo tayari kwa kuijadili  kuiboresha na hatimaye kutoka na rasimu tatu itakayopigiwa kura  ama kuikubali kuwa katiba mpya au la.

Mwanasiasa mkongwe njelu kasaka amesema hotuba hiyo imesaidia  kutoa uelewa wa mambo kwa kuwa idadi  kubwa ya wajumbe ndani ya bunge hilo hawakuwan na uelewa juu ya hoja mbalimbali  zilizopendekezwa kwenye  rasimu hiyo.

Kutokana na ufafanuni huo wengi watakuwa wameelwa kwa nini tume iliamua kupendekeza muungano wa serikali tatu na wala siyo mbili. Itasaidia pia kuwajengea uwezo wa kuhoji kaatika mijadala ya kamati itakapoanza kukaa rasmi alisema kasaka ambye alikuwa miongoni mwa wabunge 55  walioasisi kundi la G55 lililotaka  kuundwa serikali  ya Tanganyika mwaka 1993.

Lakini jambo jingine hotuba hii imeondoa  ni unafiki na imewaaibisha kwa unafiki wao baadhi y a watu kwa sababu pamoja na kuongoza serikali moja ya jamhuri ya muungano , imefahamika wazi kwamba waziri mkuu kumbe hana mamlaka yoyote yale katika upende wa Zanzibar.

Kwa upande wake profesa boniventure rutinwa wa chuo kikuu cha dar es salaam(UDSM) aliunga mkono hoja hiyo akisema kinachotakiwa  kwa wajumbe hao ni kujenga imani, kuondoa tofauti zao na kutokubaliana na hoja zenye masilahi ya vyama na makundi yao badala ya Taifa.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kupima uwezo wa kwa kuhoji je pamoja  na ufafanuzi  huo serikali tatu inaweza kuwa mwarobani wa kumaliza changomoto zote? Lakini pia wanatakiwa kufahamu kwamba inawezekana kuna changamoto nyingine ambazo zinaweza jitokeza  katika muundo huo. Alisema profesa rutinwa.

Kwa upande wake profesa penina mlama aliwataka wajumbe wa bunge hilo kuchukua hoja hizo na kufikiria kwa mapana zaidi wakati wa majadiliano ili kuondoa athari zinazoweza kujitokeza baadaye.

Wamerahisishiwa na kazi imebakia kwao kupima na kufikiria  zaidi hotuba  hii wajumbe watambue kwamba si mawazo ya jaji warioba yaliyowasilishwa pale pale ni amwazo ya watanzania ambayo yanatakiwa kupokew kwa mtanzamo chanya ili wasije kuaibika  badaye iwapo watashindwa kufanya uamuzi sahihi alisema.

Mjumbe wa bunge james mapalala alisema jaji warioba amemaliza kazi ya kuelimisha  juu ya umuhimu wa serikali tatu na anamini wataosimama kumpinga wataona haya.

0 Responses to “WARIOBA AWAKUNA WASOMI, WACHAMBUZI.”

Post a Comment

More to Read