Monday, March 10, 2014
ZAIDI YA WACHIMBAJI WADOGO WA KOKOTO NA MCHANGA WAANDAMANA HADI OFISI ZA JIJI.
Do you like this story?
Waandamanaji wakiwa na magari yao yakufanyia kazi katika ofisi za jiji |
Waandamanaji wakijaribu jinsi ya kumwona Mkurugenzi wa jiji. |
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Mussa
Zunguza akitoa maelezo kuhusu maandamano hayo
|
Afisa Mfawidhi Ofisi Ndogo ya wakala
wa Madini Mbeya Enginia Jumanne Mohamed akitoa ufafanuzi kwa wachimbaji hao
|
ZAIDI
ya Wachimbaji wadogowadogo 2000 wa uchimbaji wa madini ya kokoto
,mawe na mchanga pamoja na madereva wa maroli yanayojishughulisha na
ubebaji wa malighafi hizo wameandamana hadi kwenye ofisi za halmashauri
ya Jiji la Mbeya, kupinga uamuzi wa Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha
ushuru wa maroli ya mchanga.
Katika mazungumzo yao na Faharinews wamesema, wao hawapingani na uamuzi wa serikali wa kuanzisha udhibiti wa uzalishaji na biashara ya madini ya ujenzi na viwanda tatizo ni kushindwa kuweka wazi mfumo wa tozo la kodi kwa upande wa magari yanayojihusisha na ubebaji wa madini hayo.
Aidha,
wafanyabiashara hao waliiomba serikali kuangalia utaratibu wa kuwapunguzia
gharama ya lesseni ya uzalishaji biashara ya madini
kwani kiasi cha fedha kilichoainishwa ni kikubwa ukilinganisha na hali
halisi ya kipato cha mtanzania kwa siku.
Akijibu malalamiko hayo Afisa mfawidhi wa ofisi ndogo ya wakala wa madini Mbeya, Jumanne Mohamed, amesema kwa mujibu wa sheria zao mlipaji wa mrabaha ni mchimbaji na si dereva .
Amedai kuwa wizara kupitia waraka huo umeweka wazi kwamba mlipaji wa mrabaha ni mchimbaji na kwamba hairuhusiwi kuchimba bila ya kuwa na lesseni hivyo hii shilingi 2500 inalipwa na mchimbaji.
Amesema, mchimbaji anapolipia kiasi cha shilingi 2500 hukabidhiwa hati ya malipo ambayo hutolewa bure na kwamba hati hiyo anatakiwa kumkabidhi dereva ili asikamatwe na kutozwa faini kutoka kwa watendaji wa madini.
Amesema suala la ulipaji wa mrahaba huo uko palepale kwa mujibu wa sheria hivyo nivyema taratibu zikafatwa katika kukamilisha zoezi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZAIDI YA WACHIMBAJI WADOGO WA KOKOTO NA MCHANGA WAANDAMANA HADI OFISI ZA JIJI.”
Post a Comment