Monday, March 10, 2014

RWANDA YATIMUA MAOFISA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI.


Rais wa Rwanda Paul Kagame


Serikali ya Rwanda, imefukuza maofisa sita wa ubalozi wa  Afrika Kusini muda mfupi baada ya nchi hiyo kuwataka maofisa watatu wa ubalozi wa Rwanda kuondoka  Afrika Kusini.

Aidha, kutokana  na hatua hizo Afrika kusini imeanza kuangalia uwezekano wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia  na Rwanda, kutokana na mvutano wa siku za hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili, uliosababisha kila upande kufukuza maofisa ubalozi.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo amethibitisha serikali yake kuwafukuza Mofisa sita wa ubalozi wa Afrika kusini, kwa madai kuwa Serikali ya Afrika Kusini imewahifadhi wasi waliojihusisha na mashambulizi ya kigaidi.

“Tumewafukuza wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini kuwajibu na pia nikutokana na wasiwasi wetu kuwa nchi hiyo inawahifadhi waasi ambao wnahusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Rwanda”, amesema waziri huyo.

Afrika kusini ilichukua hatua hiyo ya kuwafukuza maofisa wa Rwanda, Baada ya nyumba ya mpinzani wa Rwanda, jenerali kayumba nyamwasa anayeishi Afrika Kusini kushambuliwa mapema wiki iliyopita jijini johanesburg.

nchini Afrika Kusini lilinukuu chanzo cha habari kutoka kitengo cha diplomasia, kikibainisha kuwa Afrika Kusini wanaangalia uwezekano wa kumrudisha nyumbani balozi wao aliyoko Kigali.

0 Responses to “RWANDA YATIMUA MAOFISA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI.”

Post a Comment

More to Read