Monday, March 10, 2014

MFUGAJI KUMVAA RIDHIWANI UBUNGE CHALINZE




Mfugaji wa ng’ombe katika kijiji cha ubena, mathayo Tolongey ameshinda katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chadema katika jimbo la chalinze, mkoa wa pwani.

Tolongey ambaye pia ni mwenyekiti wa chadema  jimbo la chalinze alitangazwa juzi baada ya kuwashinda wenzake watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Uchaguzi huo mdogo ulifanyika april 6, mwaka huu baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo said bwanamdogo kilichotokea januari 22 mwaka huu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumza kwa simu, katibu wa chadema jimbo la chalinze , Idd Ucheche amesema Tolongey aliwashinda wenzake kwa kupata kura 280 kati ya 510 zilizopigwa katika uchaguzi uliofanyika juzi.

Amesema mshindi wa pili katika kura hizo ni Omar Mvambo aliyepata kura 82 akifuatiwa na frank mzoo aleiyejinyakulia kura 57 na wa mwisho ni francis mugusa kwa kura 44.

Uchaguzi wa kura za maoni ulifanyika mjini chalinze kuanzia saa 8: 00 mchana hadi saa 3: 00 usiku na kwamba matokeo yalitangazwa na mwenyekiti wa chadema mkoa wa pwani, said ukwezi.

Ucheche alisema katika matokeo hayo kura 47 ziliharibika. Alisema waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo walikuwa sita lakini wawili walikoksa sifa baada  ya kurejesha fomu makao makuu ya chadema badala ya ofisi ya jimbo  la chalinze.

Mshindi huyo sasa anasubiri uamuzi wa kamati kuu ya chadema yenye mamlaka ya kumteua mgombea wa ubunge ili kupeperusha bendera ya chama hicho akishindana na wagombea wa vyama vingine vya siasa.

Mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo kupitia CCM Ridhiwani Kikwete naye anasubiri uamuzi wa kamati kuu kumwidhinisha kugombea nafasi hiyo.

Chama cha CUF kimeshamtangaza Fabian Leonard kwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

0 Responses to “MFUGAJI KUMVAA RIDHIWANI UBUNGE CHALINZE”

Post a Comment

More to Read