Monday, October 10, 2016
NIMEKUWEKEA HAPA FAIDA ZA KULA MATANGO NA MATIKITI MAJI.
Do you like this story?
Tikiti maji |
tango |
Ulaji wa
matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika
mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo
husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu
huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.
(1)Husaidia
kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres,
humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo
husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali
(2)Hupunguza
(hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na
unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo,
baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala,
itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers
(3)Husaidia
katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo
kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa
matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein
mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin
enzyme.
(4)Husaidia
kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo
husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo
kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha
ya kila siku.
(5)Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c,Â
(6)husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.
(7)Husaidia
kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa
dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya
kinywa na harufu mbaya mdomoni.
(8)Husaidia
mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.
(9)Huzuia
kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi wa damu
kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya moyo
(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NIMEKUWEKEA HAPA FAIDA ZA KULA MATANGO NA MATIKITI MAJI.”
Post a Comment