Monday, October 10, 2016
SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AFUMUA KAMATI YA BUINGE NA KUISUKA UPYA
Do you like this story?
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko
makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge
ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha
Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na sita wa kamati hiyo ambao
pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda Kamati za
Bunge kadri anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya yamelenga katika
kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
“Kanuni
ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 inampa
Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati mbalimbali za
Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza
idadi ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.
Mabadiliko
hayo yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe wote
wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua viongozi wa
kamati hiyo.
Hii
ni orodha ya waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo na kamati walizohamishiwa
kufuatia mabadiliko hayo:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AFUMUA KAMATI YA BUINGE NA KUISUKA UPYA”
Post a Comment