Monday, March 10, 2014

FOLENI YAZUA MARADHI MAPYA.





Wakati kukiwa na ongezeko kubwa la ununuzi wa magari na kusababisha idadi kubwa ya vyombo hivyo vya usafiri , foleni za magari nchini, hasa jijini dare s salaam imefikia hatua ya kutisha huku ikisababisha madhara makubwa ya kiuchumi, kijamii na kiafya, ikiwamo magonjwa ya akili.



Misululu ya magari ilikuwa ni ya kawaida kuonekana nyakati  za asubuhi na jioni wakati watu wakielekea na kutoka kazini, lakini sasa foleni zimekuwa ni za kawaida katikati ya jiji na maeneo mengine ambayo ukarabati wa barabara unaendelea wakati wote.



Wakati kukiwa na kasi ndogo ya ukarabati wa miundombinu ya usafiri kumekuwa na ongezeko kubwa la magari jijini dare s salaam pia kumekuwapo na ongezeko kubwa la idadi ya watu hadi kufikia 4.3 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 huku vyombo vya usafiri wa umma (daladala) vikitumia njia zisizo sahihi(kutanua) kufanya foleni kuwa kubwa hali inayosababisha jiji kuwa kero kwa muda wote.



Licha ya jitihada za serikali kutumia treni kusafirisha abiria ili kusaidia kupunguza msongamano wa magari nyakati za asubuhi na jioni bado tatizo hilo ni kubwa. Hivi karibuni waziri wa ujenzi, DK John pombe magufuri aliagiza kampuni ya strabag, inayojenga miundombinu ya mabasi yaendayo kasi kufungua barabara zilizokamilika ili kupunguza msongamano.



Kutokana na tatizo hilo, wakazi wa dare s salaam na maeneo mengine yanayoathiriwa na foleni , wamekuwa wakilazimika au kusitisha ama kuchelewa kazini na kwenye shughuli nyingine huku vyombo vya usafiri vikilazimisha kufanya safari chache na hivyo wamiliki kupata fedha kidogo kuliko matarajio yao.



“Madereva wanapata magonjwa ya akili kutokana na kero za barabarani” amesema DK innocent Godman, ambaye ni mmoja wa watalamu wa Nyanja  tofauti aliyeongea na Fahari News kuhusu tatizo hilo.


“kwanza ni msongo wa mawazo kuhusu uchumi kutokana na mafuta mengi kupotea njiani; uku barabara mbovu; tatu hasira za kuchelewa wanakokwenda; nne wanakumbana na askari wa usalama barabarani ambao wanawakamua fedha “ amesema mtaalamu huyo wa magonjwa ya akili na mshauri nasaha kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya

0 Responses to “FOLENI YAZUA MARADHI MAPYA.”

Post a Comment

More to Read