Monday, March 10, 2014

MAVAZI YA PINDA GUMZO.


Waziri Mkuu Mizengo  Pinda.


Mjumbe wa Bunge maalum la katiba John Mnyika aliibua hoja ya mavazi yanayotakwia kuvaliwa bungeni na kusababisha spika wa bunge la jamuhuri , Anne Makinda kutahadharisha kuhusu uvaaji wa suruali na shati la kitenge kama alivyokuwa amevaa waziri mkuu, Mizengo Pinda.

Suala hilo lilizungumzwa ijumaa iliyopita na liiibuka wakati mnyika akichangia kifungu cha 82 (9) cha rasimu ya kanuni za bunge hilo kinachozungumzia mavazi huku akipendekeza kuwa mavazi ya kitenge na suruali yaruhusiwe.

Mnyika alitoa pendekezo hilo na kutoa mfano wa wajumbe waliokuwa wamevaa mavazi hayo  kwa siku hiyo.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni waziri pinda, Ezekia wenje, Joshua nassari, yeye mwenyewe na wajumbe wengine kadhaa.

Hata hivyo rai hiyo ilipingwa vikali na makinda ambaye amesema kuna mavazi rasmi yanayoruhusiwa kukubaliwa bungeni.

“Yapo mavazi rasmi ya kuvaa bungeni. Mwanaume lazima avae shati na tai au suti nadhifu, sasa huu uvaaji wa mavazi yasiyo rasmi “casual” jana alivyovaa mheshimiwa pinda, hauruhusiwi humu ndani na tusiuweke kwenye kanuni” amesema makinda.

Makinda aliwataja Freeman Mbowe na Samweli Sitta kuwa walikuwa wamevaa suti nadhifu na itakuwa jambo la ajabu wakipinga wazo lake.

“Alivyovaa mnyika na mheshimiwa pinda na wengine siyo sawa” amesema makinda.

Baada ya kauli hiyo, waziri pinda alisimama huku akicheka na kuanzaa kujitengeneza vizuri shati lake la kitenge na kumnyooshea kidole makinda, kitendo kilichotafsiriwa kuwa alikuwa akimaanisha kuwa mavazi yake yalikuwa nadhifu.

Baada ya kusimama waziri pinda alinyanyuka alitoka katika ukumbi na kuzua kicheko ukumbini.

0 Responses to “MAVAZI YA PINDA GUMZO.”

Post a Comment

More to Read