Monday, March 10, 2014

MKUU WA MKOA AWAASA VIJANA KUACHA ‘KUDENDEKA.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini.


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadik amewaasa vijana kuacha tabia ya kudendeka kwani inasababisha ugonjwa wa homa ya ini.

Mheshimiwa Saidi ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya homa ya ini iliyofanyika Ijumaa iliyopita katika Hospitali ya Amana ambapo aliwataka vijana kuachana na tabia ya kudendeka hovyo kwani ni njia mojawapo inayoambukiza ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa homa ya ini ni hatari kuliko ukimwi na watu wengi hawana desturi ya kupima ili kujua afya zao hivyo vijana wanatakiwa kuacha tabia ya kudendeka hovyo kwani ni njia mojawapo inayoambukiza ugonjwa huu,”amesema Mhe. Saidi.

Aidha, amesema Watanzania wanatakiwa kutambua ugonjwa huo upo na mara nyingi kabla ya vijana kuingia kwenye ndoa huwa wanapima Ukimwi lakini wanasahau kupima ugonjwa wa homa ya ini hivyo kuanzia sasa wanatakiwa kuwa na desturi ya kupima.

Hata hivyo, aliagiza kwamba upimaji wa homa ya ini unatakiwa kupimwa katika hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam na lisiwe suala la hiyari ni lazima kwani ni mkoa ambao una changamoto kubwa ya kukutwa na ugonjwa huo kutokana na msongamano kuwa mkubwa.

Mhe. Saidi alizindua kampeni ya homa ya ini inayofikia kilele chake Julai 28, mwaka huu na hii yote ni kutokana na ugonjwa huo kuzidi kuua mamilioni ya watu kila mwaka.

0 Responses to “MKUU WA MKOA AWAASA VIJANA KUACHA ‘KUDENDEKA.”

Post a Comment

More to Read