Monday, March 10, 2014
KIJANA ATEKETEZWA KWA MOTO BAADA YA KUHISIWA KUWA NI MWIZI WILAYANI KAHAMA..!!
Do you like this story?
Kijana mmoja anayesadikiwa kuwa ni mwizi ambaye jina
lake halikuweza kufahamika mara moja amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na
Wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, katika kijiji cha Kagongwa Wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo limetokea jana majira ya Saa mbili usiku kufuatia marehemu kujaribu kukodisha Usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kwenda Kijiji jirani cha Mwankumba.
Imeelezwa kuwa madereva hao wa bodaboda walishtuka
kuona mtu huyo akiwa amevaa koti kubwa, ndipo walipomuliza ili kujua vitu
alivyobeba, na ndipo alipojaribu kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi
waliokuwepo katika eneo hilo.
Hata hivyo baada ya Kijana huyo kukamatwa amekutwa
akiwa na Mapanga mawili aliyoyaficha ndani ya koti, jambo lililopelekea
wananchi hao kuchukua jukumu la kumchoma moto wakimuhisi kujihusisha na matukio
ya wizi.
Baada ya tukio hilo Jeshi la Wilayani Kahama
limefika eneo hilo na kuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa
katika hospitali ya wilaya ya Kahama, huku uchungizi zaidi wa tukio hilo
ukiendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIJANA ATEKETEZWA KWA MOTO BAADA YA KUHISIWA KUWA NI MWIZI WILAYANI KAHAMA..!!”
Post a Comment