Monday, March 10, 2014

ETO’O AMKEJELI MOURINHO.


Samuel Eto’o



Mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto’o amemkejeli kocha    jose mourinho  aliyekuwa na hofu kuhusu umri wake, kwa kushangilia kwa mtindo wa kutembea kama “mzee” wakati waliposhinda mabao 4- 0 dhidi ya Tottenham Hotspur.

Mourinho alizua gumzo baada ya kukaririwa akisema kwamba Eto’o atakuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 32.

Baada ya kuifunga Chelsea bao na kuongoza dakika 56, Eto’o alienda   kwenye kibendera cha kona ya kupunguza mwendo na kushika kiuno huku mkono mwingine ukishika kibendera kuigiza kama wanavyotembea wazee wenye umri mkubwa zaidi.

Ushangiliaji huo uliwavutia watu wengi kwenye twitter, katika picha hiyo moja ilipata watu zaidi ya 1,000 waliochangia.

Eto’o ambaye jumatatu itakuwa ni siku yake  ya kuzaliwa. Mourinho alipoulizwa kwamba mashambuliaji wake atakuwa akitimiza miaka mingapi alijibu “nafikiri sasa atakuwa na miaka 33”.

0 Responses to “ETO’O AMKEJELI MOURINHO.”

Post a Comment

More to Read