Tuesday, March 11, 2014

MUUNDO BUNGE LA KATIBA CHANZO CHA VURUGU.


 



mtandao wa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari umesema muundo wa bunge maalum la katiba ndio chanzo cha vurugu.

Bunge hilo linaundwa na wabunge wa jamhuri ya muungano , wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar na wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali walioteuliwa na  Rais.

“Humo ndani, wabunge na wawakilishi ndio waotaka kuonekana bora kuliko wale wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete. Msingi wa kupata wajumbe uivurugwa” alisema mratibu wa mtandao huo, onesmo olengurumwa.

Amesema asilimia 75 ya wajumbe wa bunge hilo ni wajumbe wa bunge la jamhuri na wajumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar na kwamba kuwapo kwao hakutokani na ridhaa ya jamii.

“wajumbe 201 wanawakilisha makundi yote ya jamii, sasa wabunge na wawakilishi wanamwakilisha nani? Maana kama wakulima, wafugaji , wasomi , viongozi  wa dini, waganga wa kienyeji, walemavuna wengine wanawakilishwa” alihoji olengurumwa.

Alitoa mfano kwa ugnda ambako wajumbe 230 wa bunge la katiba walipigiwa kura na wananchi na mchakato wao wa katiba ulikwenda  vizuri.

Bunge la katiba linaendelea na semina ya kujadili na kupitisha kanuni za uendeshaji wa bunge, huku kukiwa na malumbano makali. Hata hivyo malumbano hayo yamekuwa yakilalamikiwa na watu wa kada mbalimbali kuwa yanapoteza muda na hata kutoishia uhai  wa siku 70 zilizowekwa na bunge hilo.

0 Responses to “MUUNDO BUNGE LA KATIBA CHANZO CHA VURUGU.”

Post a Comment

More to Read