Tuesday, March 11, 2014
LOWASSA: SIHUSIKI NA NOTI HIZI.
Do you like this story?
Waziri mkuu mstaafu,
Edward Lowassa amekuja juu kwamba
hausiki na noti zenye thamani sh 500 ambazo zimetengenezwa kwa sura yake badala
yake badala ya sura ya Rais wa kwanza wa Tanzania . Mwalimu Julius kambarage Nyerere.
Noti hizo ambazo
zimesambazwa katika mitandao mbali mbali ya kijamii kwa takribani wiki moja
iliyopita zinafanana na noti za sasa za sh 500, lakini tofauti yake ni kwamba
picha ya lowassa ndiyo inayopamba noti hiyo.
Mbali ya kusambazwa kwenye
mitandao ya kijamii noti hizo zimesambazwa kwa watu mbalimbali wa kawaida kwa
njia ya mawasiliano ya simu zao za mkononi kupitia mfumo wa whatsapp, BBM na
aina nyingine ya mawasiliano.
Haikujulikana mtu aukundi
lililochakachua noti hizo kwa kuweka picha ya lowassa wala hakuna anyejua
sababu ya mtu au kundi hilo kufanya hivyo.
Akizungumza kwa ufupi
kuhusu noti hizo zenye picha zake, Lowassa amesema hausiki kwa namna yoyote na
noti hizo yenye sura yake.
Lowassa katika taarifa
yake ya kukanusha kuhusika na noti zenye picha yake alisema kumekuwa na
muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa mahasimu wake kisiasa kumhusisha na
matukio ya uongo na kuzushia vitu vya ajabu katika mitandao ya kijamii.
“kumesambazwa picha ya
noti ya shilling mia tano yenye sura yangu (Lowassa) kitendo hicho siyo utani ,
bali ni dhihaka na dharau kwa alama za utaifa na mamlaka ya nchi” alisema
lowassa.
Kwa mujibu wa Lowassa,
anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii lakini anasisitiza
umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandano kwa kujadili kwa maendeleo
ya nchi baada ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa taifa.
Alipobanwa zaidi kufafanua
kuhusu kusambazwa kwa noti zenye sura yake, Lowassa alisema anahisi mkakati huo
umesukwa na mahasimu wake kisiasa kwa lengo la kutaka kukiamisha chama chake
cha mapinduzi.(CCM) na jamii kwa ujumla kwamba yeye ni mtu wa kuvunja kanuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LOWASSA: SIHUSIKI NA NOTI HIZI.”
Post a Comment