Tuesday, March 11, 2014

BUNGE MAALUM LA KATIBA SASA VULULUVULULU.





 Matarajio ya Bunge maalum la katiba kukamilisha kanuni kwa maridhiano yaliyeyuka tena  jana huku mambo ndani ya ukumbi yakanekana kuwa vululuvululu kwa baadhi ya wajumbe kuzungumza nje ya utaratibu na wengine kurushiana vijembe.

Baadhi ya wjumbe waliamua kutoleana lugha chafu na kuweka kando hoja za msingi zinazowafanya watofautiane na kuchelewesha kazi ya kuandika katiba mpya.

Hali ilichafuka mchana wakati wajumbe walipokutana kupitisha kanuni baada ya mmoja wao, felix mkosamali kuomba mwongozo kwa mwenyekiti wa muda, pandu ameir kificho.

 Hata hivyo kificho alimtaka kukaa chini kwa muda kwa maelezo kuwa wajumbe waliofika katika kikao hicho walikuwa wachache, hivyo mwozngozo wake kama ulikuwa unahitaji majibu ingekuwa vigumu kutolewa

Ghafla alisimama mkosamali tena na kuwasha kipaza sauti na kuhoji kitendo cha mwenyekiti huyo kumpa mbatia nafasi ya kutoa mwongozo wakati yeye amenyimwa…”mwenyekiti hivi unaongozaje kikao, inakuwaje mimi nikuombe mwongozo uninyime na mwenzangu umpe? Mwenyekiti nakuheshimu sana lakini sijui unatumia kanuni ipi kutoa nafasi kwa wajumbe wakati mimi uinizuia nisisema alihoji mkosamali.

Baada ya kauli hiyo waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu hawa ghasia aliwasha kipaza sauti na kwa sauti ya juu alisema “mtoto mdogo hana adabu” kauli hiyo ilibua hasira za mjumbe mwingine moses machali ambaye naye aliwasha kipaza sauti na kumjibu “ kubwa jinga halina adabu” kauli iliyoibua miguno ndani ya bunge.

Hata hivyo, licha ya mwenyekiti kutoa onyo kwa kauli  hiyo kwamba hazifai mkosamali alisimama katika sehemu yake na kusema kuwa hakuna mtoto mdogo na kwamba tangu lini mtoto aliishinda CCM.

0 Responses to “BUNGE MAALUM LA KATIBA SASA VULULUVULULU.”

Post a Comment

More to Read