Tuesday, March 11, 2014

FOLENI DAR: TRAFIKI MMOJA ANASIMAMIA MAGARI 1,400.




wakati msongamano wa magari nchini ukielezwa
ni moja ya matatizo ya  kiuchumi na kusababisha maradhi mengi, imefahamika kuwa wingi wa vyombo hivyo vya usafiri pia ni kibarua kigumu kwa askari wa usalama barabarani(trafiki) ambao kwa wastani kila mmoja analazimika kusimamia magari 1,400 kwa siku.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, naibu kamishna wa polisi (DCP),Mohamed mpinga alisema jana kuwa upungufu huo wa askari hutoa minya kwa madereva wasio waadilifu kuvunja sheria za usalama barabarani na kusababisha foleni zisizo za lazima na wakati mwingine ajali.

Akizungumza kuhusu msongamano huo unaoifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu afrika baada ya afrika kusini na Uganda, mpinga alisema shughuli kubwa kwa askari hao kutumia muda mrefu kuongoza magari iko katika jiji la dare s salaam ambalo lina zaidi ya nusu ya magari yalipo Tanzania.

“Tanzania kuna magari yapatayo milioni 1.3, kati ya hayo 700,000 yapo dare s salaam. Ndiyo maanda foleni inakuwa tatizo sugu la jiji  hili”. Alisema mpinga na kubainisha kuwa askari waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za barabarani ni takribani 500, ikimaanisha kuwa kila mmoja anasimamia wastani wa magari 1,400.  

0 Responses to “FOLENI DAR: TRAFIKI MMOJA ANASIMAMIA MAGARI 1,400.”

Post a Comment

More to Read