Tuesday, March 11, 2014

VITUKO VYA KEISSY BUNGENI.




Katika hali inayoonekana kuchoshwa na miongozo, hoja na michango inayotolewa mara kwa mara na wajumbe wenzake wa bunge maalum la katiba. Ally Keissy, amebuni dawa ya kukomesha hali hiyo.



Tangu kuanza kwa bunge hilo. Kazi kubwa ilikuwa ni kujadili rasimu ya kanuni ambayo ina vifungu 87.



Hata hivyo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakisimama na kutumia kipaza sauti na kama  mjumbe mwingine naye atawasha kipaza sauti chake hakuna anayeweza kuzungumza.



Huo nio mchezo unaofanywa na keissy kutokana na kitendo cha baadhi ya wajumbe kuonekana kuwa wachangiaji wakubwa katika mjadala huo.



Mwenyekiti wa bunge hilo, naye anaweza kuzima kipaza sauti cha mjumbe yeyote kama akiona inafaa.



Mara nyingi amekuwa akifanya hivyo wanaposimama wajumbe waochangia mara kwa mara akiwemo , Christopher ole sendeka. Ezekiah oluoch, john mnyika , Julius mtatiro na mara kadhaa wakisimama eziel wenje , ummy mwalimu na Joshua nasari.



Keissy pia anafanya hivyo wanaposimama wajumbe wengine wanozungumza zaidi utani vichekesho na kukera wenzao.

0 Responses to “VITUKO VYA KEISSY BUNGENI.”

Post a Comment

More to Read